THE HIDDEN POWER.!!
By Malisa GJ,
Mwaka 1836 binti mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 18 kutoka familia ya
kitajiri huko Lexington, Kentucky alimuomba Mungu aolewe na Rais wa
Marekani. Licha ya kwamba utajiri wa familia yao ulitokana na biashara
ya utumwa lakini wazazi wake waliamua kuachana na biashara hiyo mwanzoni
mwa miaka ya 1800's na kuwa wacha Mungu.
Mary alikuwa muumini wa makanisa ya uamsho kwa wakati huo
(Presbyterianism), kama ilivyo makanisa ya kiroho leo. Siku moja
akamwabia baba yake, "Mungu ameniambia kuwa mwanaume wa maisha yangu
atakuwa Rais wa nchi hii".
Baba yake akastaajabu, lakini hakutaka kumkatisha tamaa. Akamwambia
"binti yangu, nchi hii ni kubwa sana, na wasichana wengi wangependa
kuolewa na watu mashuhuri na wenye madaraka, lakini si jambo rahisi
kuolewa na Rais. Na ukisubiri hali hiyo kutokea unaweza usiolewe kabisa
katika maisha yako".
Lakini yule msichana akamtizama baba yake kisha akamjibu "sijali ni
wasichana wangapi wanaotamani kuolewa na watu mashuhuri, sijali nchi hii
ni kubwa kiasi gani. Ninachojali ni kuwa Mungu ameniambia kuwa siku
moja nitakuwa first lady wa nchi hii. Hilo tu"
Maka mmoja baadae (1837) yule binti akachumbiwa na mwanasiasa machachari
chipukizi aliyekuwa mwanasheria na mbunge wa Illinois (the rising young
lawyer and Democratic Party politician) aitwaye Stephen Douglas. Kwa
kuwa Stephen alikuwa mbunge, baba wa yule binti aliamini kuwa huyo ndiye
angemuoa mwanae na angekuja kuwa Rais wa Marekani baadae. Kwahiyo ndoto
za binti yake zingetimia kupitia Stephen.
Lakini miaka miwili baadae (1839) uchumba wao ukavunjika.
Mwaka huohuo (1839) katika mji wa Springfield, Illinois, yule binti
akakutana na kijana mmoja msomi wa sheria lakini kutoka familia maskini
huko Indiana. Kijana huyu alikuwa amekuja Illinois kutafuta kazi. Wazazi
wake walikua wakulima maskini. Ardhi yao huko Kentucky ilitaifishwa na
hivyo wakahamia Indiana.
Kijana huyu akapendana na yule binti na kuamua kuoana. Mwaka 1840 mwezi
December kijana akamvisha pete ya uchumba yule binti. Baba wa binti
hakufurahishwa. Akajiuliza iweje mwanae amkatae "mbunge" na akubali
kuolewa na "mtoto wa mkulima??". Kwa masikitiko akamuuliza binti yake
"unakumbuka ahadi ya Mungu kwako?". Binti akajibu "hata sasa bado
naamini."
Miaka minne baadae (1843) wakafunga ndoa.
Miaka 17 baadae (1861) yule kijana akachaguliwa kuwa Rais wa 16 wa
Marekani. Jina lake aliitwa Abraham Lincoln, na mkewe aliitwa Mary Todd
Lincoln.
Mary ndiye aliyekataa kuolewa na Steven Douglas (Mbunge) kwa ajili ya Lincoln (mtoto wa mkulima).
Baba yake Marry akiwa mzee wa zaidi ya miaka 80 alishuhudia mwanae akiwa
"First Lady" akamwambia "Mungu wako ni mkuu sana. Aliahidi na
ametimiza". Mwaka mmoja baadae (1862) mzee Robert Todd (baba yake Mary)
akafariki.
MORAL OF YHE STORY.!
Hadithi hii ni ya kweli kabisa inayomhusu Rais Abraham Lincoln na mkewe Mary Todd Lincoln. Kuna mengi ya kujifunza kwenye kisa hiki, lakini ningependa kukushirikisha machache niliyojifunza mimi.
Hadithi hii ni ya kweli kabisa inayomhusu Rais Abraham Lincoln na mkewe Mary Todd Lincoln. Kuna mengi ya kujifunza kwenye kisa hiki, lakini ningependa kukushirikisha machache niliyojifunza mimi.
#Lesson_1:
Ukiomba usichoke kusubiri. Mungu akisema atakupa, basi amini atakupa
tu. Mungu wetu ni mwaminifu na hutupa kwa wakati wake. Mary aliona maono
ya kuwa first lady akiwa na miaka 18, lakini ilimchukua robo karne
(miaka 25) hadi maono yake kutimia. Sasa wewe ndugu yangu umemaliza chuo
mwaka jana umeomba kazi hata mwaka haujaisha umeshaanza kumlalamikia
Mungu. Subiri. Au umeomba mchumba mwaka wa 3 hujapata, unaanza
kumlalamikia Mungu eti wenzio wote wameolewa/kuoa. Tafadhali subiri.
Mungu atakupa kwa wakati wake unaofaa.
#Lesson_2:
Ishi katika misimamo. Baba yake Mary Todd alipoona mwanae amemuacha
"Mbunge" akaolewa na Mtoto wa mkulima alimuona kama vile amepoteza dira.
Lakini binti alijua ipo siku Mungu atatenda. Na Mungu alivyo mwaminifu
hakumruhusu baba yake Mary kufa kabla hajashuhudia Mwanae akiwa "first
lady" wa Marekani. Point hapa ni kwamba jifunze kushikilia imani yako na
uwe na msimamo usioyumba hata kama dunia nzima itakuacha. Wengi
waliobarikiwa ni wenye misimamo. Jifunze kuwa focused and visionary.
Usitazame vinavyong'ara leo, tazama vitakavyong'ara milele.
#Lesson_3:
kuna kitu kinaitwa "Hidden Power" yani nguvu iliyofichwa. Ni nguvu
ambayo unakuwa nayo wewe lakini inatokana na watu wengine. Unaweza
kufanikiwa sana, lakini si kwa juhudi zako bali kwa sababu nyuma yako
kuna watu wanaofanya wewe ufanikiwe. Wanakuombea, wanafunga kwa ajili
yako, wanamsihi Mungu kwa ajili yako, wanaomba ulinzi, baraka, na neema
kwako. Wanaweza kuwa wazazi wako, mwenzi wako, watoto wako, rafiki zako,
ndugu zako etc.
Lincoln alikuwa na nguvu iliyofichwa kupitia mkewe. Yani mke wa Lincoln
(Mary) ndiye aliyemfanya mumewe kuwa Rais. Kama Lincoln asingemuoa Mary
Todd asingekuwa Rais wa Marekani. Na hata Lincoln mwenyewe aliwahi
kukiri kwamba "Urais haukuwahi kuwa ndoto zake katika maisha"
#Lesson_4:
Our GOD is the GOD of imposibilities. Yale tunayoona na kudhani
hayawezekani, kwa Mungu yanawezekana. Wakati Mary akiwaza atakuwa first
lady wa Marekani, Lincoln hakuwahi kuwaza kama angekaa awe Rais. Sijui
kama unauona ugumu huu.! Imagine Mungu anakuahidi utakua "first lady",
halafu anakataa usichumbiwe na Mbunge. Anakupa mchumba mwingine, halafu
huyo mchumba anakwambia "sina hata ndoto za Urais". Ingekua ni wewe
ungejisikiaje? Wengine mngemlaumu Mungu na kutamani kurudi kwa mbunge,
right? Lakini Mungu akiahidi ni lazima atimize.
#Lesson_5:
Mungu huinua vyenye nguvu katikati ya vinyonge. Unakumbuka hadithi ya
Daudi? Yesse alipoambiwa aite watoto wake wote maana mmoja wao atakua
Mfalme, aliita wote akamsahau Daudi. Imagine baba yako mzazi anakusahau.
Lakini Mungu akamfanya huyohuyo mdogo, mnyonge, aliyesahaulika kuwa
Mfalme. Lincoln nae pengine alionekana mnyonge, lakini Mungu akasema
"huyu ndiye"
Katika maisha usimdharau mtu yoyote. Heshimu kila mmoja. Unayemdharau
leo aweza kuinuliwa kesho ukabaki unashangaa. Ipo nguvu iliyofichwa (the
hidden power) kwa kila mmoja wetu. Unaweza usiione nguvu hiyo leo
lakini ipo siku itafanya kazi.
The hidden power.!!!
0 comments:
Post a Comment