Heri ya Mwaka Mpya 2018. Si makusudi yangu kusifia Uhalifu lakini katika Ulimwengu huu kuna akili za ziada au vipaji ambavyo watu wanavyo sema tu matumizi yake ndo huwa yanakuwa ya kihalifu. wazungu wenzetu bado hukaa chini na kutathmini faida na hasara ya akili za watu flan flan hata kama walikuw awahalifu. leo hii tunamzungumzia Frank Williams Abagnale Jr ambaye baadaye FBI ilibidi wamwajiri baada ya kumkamata na kustaajabishwa na uwezo aliokuwa nao.
Kwa wale ambao wamewahi kutizama movie inaitwa Catch me if You Can au kusoma kitabu chenye jina hilo hilo bila shaka watakuwa wamewahi kusikia kisa cha Tapeli/Msanii mmoja mwenye akili kuwahi kupata kutokea Duniani. Huyu jamaa aliyekuwa akifahamika kwa jina la Frank W. Abagnale Jr. Akiwa na miaka 15 alianza shughuli za kufanya utapeli au usanii kiasi kwamba mama yake ilibidi mapeleke shule ya watoto watukutu. Frank alipomaliza shule aliamua kutafuta ajira hasa baada ya baba yake kuyumba kiuchumi na kusababisha awe na maisha magumu. vyuma vilikaza.
Frank aliamua kuondoka nyumbani akiwa na checkbook pamoja na Usd 200 katika account yake akielekea New York City kutafuta maisha. Akiwa huko akawa anaishi na familia ya kijana mmoja ambaye walikutana kwenye train wakati wa safari yake basi akamuuzia uzia chai wakawa marafiki na badaye akafikia kwao. Haikuchukua muda mrefu alifanikiwa kupata kazi katika kampuni moja ya stationery akitumia uzoefu alioupata aliupokuwa akifanya kazi katika kampuni ya baba yake.
Frank aligundua ilikuwa ngumu sana kuishi maisha mazuri katika jiji la new York hasa hasa ukiwa hujasoma angalau kuwa na elimu ya kwa ngazi ya Diploma. Na ili kuweza kuishi vizuri pale jijini basi alipaswa angalau aweze kupata zaidi ya Usd 1.50 kwa saa kiasi ambacho alikuwa akipata. Hivyo alianza kuchangamsha akili kuwa afanye nini ili aweze kuongeza kipato.hakuchagua kuwa punga.no. alichagua kuwa Msanii. Alifanikiwa kupata wazo ambalo lingemsaidia kupata kipato cha ziada na hivyo kusababisha miezi ikutane.
Akaamua kuchezea leseni yake ya udereva. Ambayo mara ya kwanza ilikuwa inaonesha alizaliwa mwkaa 1948 akarudisha nyuma na kuifanya ioneshe amezaliwa mwaka 1938. Miaka 10 zaidi ya umri wake.hii mbinu ilifanya kazi.watu walikuwa wakimwona ni mtu mzima kutokana na yeye kubehave na kuonekana hivyo na pia hata urefu wake wa futi 6 na mvi za urithi ambazo zilikuwa zimeanza kumtoka.basi ilikuwa ni rahisi kumdhania kuwa ni mtu mzima. Frank hakuishia hapo. Kaanza kujifanya kama ni mtu ambaye amesoma sana akijua hii ingemsaidia katika kuongeza mshahara wake. Hata hivyo aligundua hata pamoja na kufanya sarakasi zote hizo yaani za kuongeza umri na kudanganya kuhusu elimu yake bado hakuweza kupata pesa ambayo ingemsaidia kuishi maisha mazuri kama alivyokuwa ametegemea.akaamua kuchemsha tena akili.
Atafutaye hachoki. Frank alikumbuka kuwa alikuja New York akiwa na chekcbook na alipofika new York alifungua check account kupata blank checks. Akadhamiria kutumia hizo checks kwa hali ambayo ingempa faida Zaidi kuliko ambavyo ilikusudiwa.yaani kufanya usanii/utapeli.
Frank akafanya maamuzi magumu. Akaamua kuacha kazi na kuanza kufanya utapeli kwa Mabank kwa kujiandikia check feki. Alishafanya jambo hili hapo kwanza na hivyo akawa ameendeleza huu mchezo wa kujiandikia check feki na kuvuta mapene kutoka bank.akijipatika Madollar kibao. Lakini alishtuka kuwa si muda mrefu mapolisi watakuwa wanafaham mchezo wake hivyo akaamua kuondoka kwenda sehemu nyingine na kubadilisha jina.
Mpango wa Kujifanya Rubani wa Shirika kubwa la Ndege Duniani.
Frank W akiwa na mtoto mmoja mkali baada ya kutoka kumgegeda.
Alipata wazo la kujifanya rubani hasa baada ya kushuhudia mara nyingi marubani walivyokuwa wakipata heshima katika jamii. Alishashuhudia marubani wengi wakiwa nje ya Hotel ya Commodore wakila bata na mademu wakali wa kibongo,kitasha,kihindi,kiarabu na kilatino aka admire sana ile life style na siku zote alikuwa akiwaza maisha yale ya kula bata kwa kwenda mbele.Na akaona ili sasa aweze kuzi cash zile bad checks zake bila bugudha au kutiliwa mashaka basi inabidi ajifanye naye ni rubani. Hapo tayari alikuwa ameshaziandika cash kadhaa ambazo inabidi akazi cash.
Basi akaamua kupata sare za marubani wa Shirika la ndege la Pan Am (Pan American) na kujifanya yeye ni mmoja wa Marubai wa Panam. Akaanza kufanya mchakato mtoto wa mjini… wanasema "kuku hafi kwa utitiri "na ndivyo ilivyo kwa mtoto wa mjini hafi kwa njaa. Akampigia simu wakala wa manunuzi wa Pan American Airlines Corporate makao makuu na kuwaambia kuwa yeye ni Rubani(pilot) wa Kampuni hiyo ya Panam na kuwa katika Hotel aliyokuwa anaishi walipoteza Sare yake ya kazi. Jamaa kule wakamwambia hamna noma basi aende kuchukua hiyo sare katika Kampuni ambayo wao wame specialize katika kutengeneza uniform za Pan Am mtaa wa 5th Avenue. Naye pasipo kuchelea alifanya hivyo. Siku hiyo hiyo aliafanikiwa kupimishwa Sare na akawapa namba ya Mfanyakazi ambayo aliibuni alipokuwa akijaza form.
Hatimaye frank alitoka katika lile jengo akitabasamu kimoyo moyo akiwa ameshikiria sare yake mkononi akiwa amefanikiwa kuvuka kikwazo kimoja wapo katika mchakato wake. Ili sasa kujihakikishia nafasi ile akaamua kutengeneza na kitambulisho cha Pan Am. Baada ya kuangalia katika vile vitabu vya simu maarufu kama Yellow Pages frank aligundua kuwa 3M ndo ilikuwa Kampuni inayohusika na utengenezaji wa Vitambulisho kwa Makampuni Mengi ya Ndege ikiwepo Pan Am. Akawasiliana na kampuni hiyo akijifanya yeye ni Afsa manunuzi ambaye amedhamiria kutengeneza vitambulisho vipya kwa ajili ya Kampuni yake. Akaomba wakutane na mhusika wa 3M kwa ajili ya maongezi Zaidi. Akakutana na afsa wa Kampuni anayehusika na mauzo na huko akapewa catalogs mbalimbali za vitambulisho walivyo navyo.katika hilo akagundua kitambulisho ambacho kinafanana na vinavyotumiwa na Pan Am. Akamwambia mhusika wa ile Kampuni alitaka apewe copies za sample za vitambulisho ambacho kitawekwa picha na details zake kama mfano ili akawaoneshe wafanyakazi wenzie vitambulisho vile vitakuwaje. Kitambulisho kile kilifanana kabisa na vile vya Pan Am isipokuwa ilikosekana Logo tu.akatengenezewa akachukua akawaoneshe wafanyakazi wenzie kama alivyojinasibu kwa yule jamaa.
Frank alitatua tatizo hilo la kukosekana nembo kwa kuamua kununua mfano wa ndege ya Pan Am. Yaani toy ambapo katika hilo akanyofoa hiyo alama ambayo ni famous sana na kwa umakini akaibandika kwenye kitambulisho chake na kilionekana kama vile vile ambavyo vinatumika na maruban wa Pan Am. Kikwazo kingine akawa amekivuka. Sasa ana sare na kitambulisho. Safari yake ya kuelekea kula bata ikawa inazidi kukaribia.
Akawa amaebakiwa na maeneo mawili Zaidi ya ku clear. Alitakiwa kuwa na leseni ya FAA ambayo kila rubani anapaswa kuwa nayo na pia awe na ufahamu kuhusiana na shughuli za Airlines. Kwanza akaamua kutafuta habari nyingi kadri awezavyo kuhusiana na usafiri wa anga,urubani na pia maneno au terminologies ambazo zinatumika katika kada hii ya usafiri wa anga. Akaanza kuwa anaingia library kujisomea ingawa alikuta vitabu vingi vimekuwa outdated.lakini alijitahidi kupata ABCs za Urubani.
Akaona ili kuweza kupata habari za uhakika na za kuaminika basi aanze kufanya utaratibu wa kupata habari hiz kutoka kwa wahusika wenyewe yaani wafanyakazi na marubani.akaanza kuandaa mahojiano na wafanyakazi wa Pan Am akijifanya yeye ni mwanafunzi anayefanya research project kuhusiana na kampuni hiyo na marubani wake. Lilikuwa ni wazo bora kabisa lenye akili. Alijipatia utajiri wa habari za uhakika pamoja na ufahamu kuhusiana na sera,kanuni na taratibu kama msaidizi wa rubani. Co-pilot. Aina ya ndege zinazotumika na njia za kimataifa zinazotumika.jamaa akawa fiti sana katika eneo hilo.
Zaidi Zaidi alipata kufaham kuhusiana na deadheading. Deadheading ni mfanyakazi wa ndege ambaye anapata kipaumbele cha kusafiri kwa kutumia ndege nyingine kwenda sehemu mbalimbali bure kwa ajili ya kwenda kufanya shughuli flani. Mwajiri ndo anayelipia hii safari kwa kila kitu.hapa frank alitasabamu na kuona sasa ameuchinja.maana akiwa kama rubani pia deadheading atakuwa sometime anasafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani kwenda kula bata akilipiwa na kampuni. Mungu ampe nini Frank? Upele? Elimu yote hii aliihifadhi kichwani mwake akiendelea kujikita Zaidi katika kukamilisha mpango wake.
Issue iliyokuwa inafuatia sasa ilikuwa ni kupata leseni ya FAA aligundua kuwa bila leseni hiyo asingeweza kujifanya yeye ni rubani.sababu wakati mwingine marubani walitakiwa kuonesha leseni ya FAA ikiwa angepanda ndege nyingine kama Staff yaani deadheading. Si unajua zile za kibongo hata kwenye daladala wakati konda akidai mchango wa mafuta utasikia “mi stafu” basi ndo na wao ili uonekane staff basi sometime utaulizwa tuoneshe leseni yako ya FAA. Frank aligundua FAA walikuwa na Branch hivyo akajiita Frank Williams na kuwa ametumwa akachukue documents za maelezo ya vitambulisho baada ya kutumiwa mail ndugu yake ambaye ni rubani. Akachukua ule mfano wa vitambulisho toka kwenye barua na vipeperushi vya FAA akaiweka kwenye printer na kuifanya iwe ndogo akaibandika kwenye karatasi maalum na kulaminate. Shabash ! frank alikuwa tayari ameshaula.huwezi amini ilikuwa copy right kama zile zile za marubani.alitabasamu tena na kurusha ngumi hewani ya kujipongeza huku akianza kufurahia jinsi ambavyo atakuwa anakula bata na watoto wakali.
frank akiwaza amezungukwa na watoto wakali.
Frank sasa alikuwa amekamilika.ana kila kitu. Leseni ya FAA, leseni ya urubani, Sare na Ufaham kuhusiana na kazi hiyo. Yaani kifupi alikuwa yupo Gado Ile mbaya. Ukimcheck hivi we mwenyewe unaingia King kuwa jamaa ni Rubani..mkipiga stories za mambo ya huko hewani ..unaweza jikuta una come jinsi alivyokuwa fresh.
Safari tayari ya kuanza kula bata na kutapeli Mabank duniani
Basi mshkaji akakaza mwendo akiwa ametinga sare zake za kirubani na vitambulisho vyake vyote akiwa anatumia jina la Frank Williams akaenda mpaka Bank kwenda kufungua Account akiwa ametinga sare au uniform za marubani akitembea kimikogo kabisa kwa kujiamini. katika mabenk yote aliyopita walikuwa wakimheshimu sana maana miaka hiyo ya 1960s marubani walikuwa wanatesa sana kitaa...kama una demu wako hajielewi elewi trust me rubani angeweza kukupora kirahisi sana akamgonga akakuachia maumivu. yaani walikuwa wanaonekana mambo safi sana na wanaheshimika ile kinoma.tena Zaidi yeye kutoka Kampuni kubwa ya kimataifa. hawakujua. hawakujua maskini, kuwa huyu alikuwa bwana mdogo tu tapeli msanii wa kiwango cha standard gauge.
Frank akawa amekuwa mcharo ile mbaya. Mademu wengi walikuwa wakimzimia..hasa wale mademu wafanyakazi wa kwenye ndege na si unajua walivyo wakali… basi wengi wakawa wanamjia tu kwa nyuma "frank tunakuzimia" n.k. jamaa hakuwanyima haki yao.akawa anawapa tu.anawapa, anawagaia,anawakita na mashine,anawapa mkono,akawa anawacharaza bakora,anawapiga kwa ukuni...si unajua ukishakuwa mwana utamaduni humchapi mwanamke kwa fimbo...unamchapa kwa ukuni.watu wa kale toka zamani.... Ikawa yeye ni mtu wa kuwa na list. Anatick tu huyu tayari, huyu tayari..huyu bado next week. Kumbe aogope nini na uzushi upo pembeni?
Kwa kujiamini kabisa akaamua kusafiri kama deadheading kuelekea Miami..si umewahi zisikia beach za Miami ?(tamka mayami) alipanda pipa ndege ya Eastern Airline 127 akiwa na sare zake na kujaza form akiweka details zote. Akiwa huko ndani akaenda mpaka kukaa sehemu inaitwa cockpit huko alikaa kwenye seat na kuwa tayari kwa swali lolote ambalo angeulizwa na marubani. unajua kosa moja tu lingemfanya wamshtukie na wampeleke segerea kunyea debe? Jamaa alikuwa anajiamini ile mbaya akakaa mle ndani ame chill tu kama mtalaam ile kinoma.
Kinyume na matarajio yake marubani wala hawakujishughulisha naye kule mbele kwenye chumba chao mwishowe wakatua Miami na hapo akashusha pumzi za kushukuru..afadhali.kutoka hapo Frank akagundua sasa atakuwa kila mara anasafiri kama deadheading kwa miaka kadhaa ijayo.ilikuwa bure na alikuwa anaweza kwenda sehemu yoyote ya dunia ambako angeenda ku cash zile check zake fake. Jamaa akawa anakula bata tu na watoto wakali toka mataifa mbalimbali. Wakati anahojiwa anasema hivi vitu vitatu vilimsaidia sana katika shughuli zake za utapeli hapa duniani.1. mwonekano wake 2. Umakini wake katika kutambua mambo 3. Kufanya utafiti wa kina kabla ya kufanya jambo lolote.
Anasema alijifunza jinsi ya kuweza kutapeli kwa kupitia cash baada ya kufanya utafiti kwa kuangalia details flan flan kwenye check. Na kuhakikisha kuwa anazichezea hizo namba katika namna ambayo itachukua muda sana kugundua kuwa zile namba zimechezewa check ni fake. Hivyo alikuwa akiziandika zionekane ni za mbali sana ili zichukue muda mrefu kufuatiliwa na hvyo kumfanya aweze kujitolea pesa tena na tena katika bank hiyo hiyo.
Zaidi Zaidi frank alikuwa anafanikiwa sababu alikuwa pia anafungua akaunt ya ukweli kwa jina la kufikirika.na mara kadhaa alikuwa akitumia check deposit ya ukweli na kuwapa bank address ambayo alikuwa kiishi au sanduku la barua ambalo angepokea check husika. Hizo information zilikuwa zinafanya transaction iwe ya kuaminika kabisa.akawa anajiandikia check kwa jina lingine na kwend ku draw pesa katika banks mbalimbali hapa duniani. Inawezekana hata bongo alifika…(ila sidhani miaka hiyo tulikuwa bado sana). Na pale bank husika ilipokuja kugundua kuwa check ilikuwa ni fake yeye alikuwa tayari ameshaondoka yupo pande nyingine ya dunia...
..................................................................................................................................
SEHEMU YA PILI
Frank aliendelea kuishi maisha haya ya kuhama hama na kuwakwepa mapolisi kila sehemu huku akiendelea kula bata na watoto wakali. Kiufupi maisha yalikuwa yamemnyookea hasa, ingawa alikuwa anaishi kwa mashaka kiasi flani lakini alikuwa smart sana. Maelfu ya dollar alizokuwa anatapeli kwenye mabenk alikuwa anazificha kwenye masanduku salama ya kuhifadhia pesa (safe deposit boxes) kila sehemu ya nchi ili hizo pesa zitumike ikiwa atapata msala. Alishajua kuwa amechagua kuishi maisha ya namna hiyo hivyo anapaswa kuwa tayar tayari wakati wowote akipata msala. Mtu mwingine ungefikiria kuwa jamaa jinsi alivyokuwa na pesa ana anavyokula bata na mademu kila sehemu alikuwa ana enjoy sana. Hapana. Alifikia hatua akachoka maisha ya kuwakwepa mapolisi na akawa wakati mwingine anakuwa mpweke sana.kwenye mahojiano anasema kila mtu aliyekutana naye hakuweza kudumu naye maana alikuwa anajitambulisha kwa fake name. si jina lake halisi.hivyo akawa hadumu na marafiki. Mademu anagonga tu halafu anaanza mbele hataki kudumu na demu muda mrefu maana ilikuwa ni risk sana.”hivyo ye anapita tu” ....
Frank alishajua kuwa yale maisha hayakuwa ya kudumu hivyo alikuwa anaishi kwa umakini sana lakini alijua kuna siku tu angekamatwa. Kweli siku hiyo ilifika. Alikuwa akisafiri kuelekea Miami akiwa kwenye ndege kama kawaida deadheading..yaani anasafiri bure. Ndege aliyopanda ikatuka Dade County na akiwa ndani ya ndege maofisa wa polisi watatu wakamfuata na kuanza kumhoji. Yeye alikuwa amejenga utulivu mzuri tu akidai kwa kujiamini kabisa kuwa yeye ni Frank William na kuwa ni Pilot bado wale maofisa walimchukua kwa ajili ya mahojiano Zaidi.
Akiwa anahojiwa frank akatoa kitambulisho chake fake na kwa kuwahakikishia kabisa akawapa majina ya marubani,wafanyakazi,masela kibao wa kazini wengine wa PanAm aliokuwa anafanya nao kazi. polisi walipowapigia jamaa hao waliwahakikishia kuwa jamaa ni mwana/mfanyakazi mwenzao wapo naye kitambo tu wanapiga naye mzigo PanAm bila shida yoyote tena mtu peace sana hana noma wala kokoro. Na Frank alikuwa mjanja sana aliweza kujichanganya na wenzie kila alipokuwa akisafiri na wakamwamini kuwa ni Rubani kweli kweli. Polisi walipopata huo uthibitisho kwa masikitiko, wakamwomba msamaha kwa kumsumbua na kumchelewesha. Akawaambia wasijali anajua wapo kazini na dunia imeharibika hivyo wanatimiza wajibu wao. hamna noma peace and love.na polisi walihisi pengine angeweza washtaki kwa kumharass..jamaa aliwahakikishia yale yamepita na yaliyopita si ndwele wagange yajayo...wakapeana tano na mapolisi akaondoka zake.kuanzia hapo akaamua kutulia kwanza kidogo kwa muda flan kwa kiingereza tunaita ku lay low for a while. Atulie kwanza kucheck hali ya hewa.
FRANK AWA DAKTARI WA WATOTO
Akiwa Atlanta Frank alifanikiwa kupata eneo flan limetulia sana ambalo vijana wengi walikuwa wamechukua apartments akaamua naye apange eneo hilo kwa mwaka mmoja. Na huko alijiandikisha kama ni doctor akiwa anajaza mkataba wake wa kupanga hizo apartment. Na kudai ni daktari ambaye alikuwa amekuja kupata mapumziko ya mudA mrefu kutokana na kupiga kazi kwa muda kwa miaka mingi akiwa daktari wa watoto yaani pediatrician. mshkaji alikuwa msanii kinyama.
Basi jamaa akawa amejenga utulivu maeneo hayo.anakula tu pesa zake za kuwaibia mabenk.wewe unahangaika kuwatapeli waswahili wenzio maskini laki laki zao.mwenzio anayaibia mabenki hata dhambi hapati sana.uongo? Siku moja ametulia home anacheck zake movies akasikia hodi. Kwenda kufungua akakutana na jamaa mmoja ambaye alijitambulisha kuwa ni doctor. Frank akaona huu sasa msala kakutana na doctor mubashara kabisa kaja kumtmbelea.maana alijua ishu yake ingebumbuluka.wakiwa katika maongezi alijitahidi sana kutengeneza utulivu na mwishowe akaja kugundua yule doctor hakuwa interested sana kuzungumzia masuala ya kazi.alikuwa alikuwa mtu wa watoto sana… hivyo huko kwenye mademu sasa ndo akamkuta frank kwenye profession yake kabisa aliyozaliwa nayo...sehemu husika .. wakawa wanapiga sana stories kuhusu mademu na kuanza kuwagonga ..wakagundua wote ni wazee wa mabinti na hivyo wakawa marafiki sana.
Yule doctor akamwomba Frank siku moja amtembelee katika hospital anayofanya kazi.pasipo kigugumizi frank alikubali. Na ikawa anamtembelea kila mara na mwishowe frank akawa anafahamiana na wafanyakzi wengi tu pale hospitalini. Si unajua mtoto wa mjini anavyojichanganya haraka na watu.hii ilimsaidia sana maana aliweza sasa kujifunza juujuu kuhusiana na udaktari wa watoto.mwishowe hata aliruhusiwa kuwa anaingia library huko alijitahidi sana kujifunza udaktari wa watoto kama ambavyo alikuwa akijinasibu.
Jamaa alionekana kufit sana kwenye hii nafasi alionekana anaipenda sana kazi na mwishowe siku moja meneja wa ile hospital akataman aonane na frank waongee kuhusu ajira pale kazini. Yaani alimpenda frank akapenda naye afanye kazi katika ile hospital. Dah…. Frank akaona huu sasa msala,ishakuwa noma.maana hakuwa daktari wa ukweli Zaidi ya usanii tu.akawa anajaribu sana kukwepa hiyo hali lakini jamaa alikuwa akimsumbua kila wakati kuwa waonane waongee. Mwishowe akakubali. Na yule meneja akamwambia kitu ambacho zaidi kikamshangaza frank.alimwomba kuwa awe anasupervise wanafunzi wa udaktari wanaokuja mafunzoni shift za usiku kuchukua nafasi za daktari ambaye alikuwepo aliyepata dharura.frank alikataa… lakini meneja alimshawishi sana.kabla ya hapo frank alikuwa amepewa nafasi ya kuwasimamia wagonjwa mbalimbali pale hospitalini baada ya kuwa amepata kibali cha kufanya kazi Jimbo la Georgia.
Frank alikuwa na ujanja flan kukwepa maswali ambayo alikuwa hayafaham pindi aulizwapo. Ikiwa ingetokea angeulizwa kitu ambacho hakijui basi angekifanyia mzaha au utani na mwishowe kingepotezewa.yaani ilikuwa huwezi mbananisha kwenye maelezo ambayo hayajui...atakuuzia uzia chai mtacheka ishu itapita. Basi baada ya kuachia ile kazi ya usimamizi wa wagonjwa kwa mhusika mwingine siku zote ule uwezo wake wa kufanya masikhara na utani vilimsaidia sana kuficha ukweli kuwa hakuwa amesomea udaktari. Zaidi zaidi wafanyakazi wengi walikuwa wakimpenda maana alikuwa mtu wa chai sana na ucheshi kuwafanya wacheke muda mwingi kumbe mshkaji ndo anafukia fukia mashimo kwa style hiyo.hakuwa na beef na mtu wala ujivuni.alikuwa mtu wa watu sana.Basi aliendelea ku maintain ile nafasi yake kama daktari msimamizi sababu hakuwa akilazimika kufanya kazi yenyewe Zaidi ya kusimamia inavyofanywa na madaktari wengine.
Siku za mwizi ni arobaini. Siku moja mtoto aliletwa chumba cha wagonjwa wa dharura akiwa amejeruhiwa mguu.frank akaitwa kwenda kusaidia. Naye aligundua hapo ndipo rangi yake itajulikana kama ni nyekundu au njano.akaona isiwe shida haraka naye akawaita wale vijana waliokuwa mafunzoni akawakabidhi ile kazi halafu yeye akasimama serious kuwaangalia wakipiga kazi.huku akikagua kagua.nao kwa kutaka kupata sifa kwa msimamizi wao ambaye ni frank wakapiga ile kazi vizuri sana. Lakini jambo hili lilianza kumpa shida kiasi kikubwa sana. Sasa alianza kuwaza kuwa anacheza na maisha ya watu hivyo akaona si suala la kulifanyia mchezo. Frank akaamua kuondoka hapo hospitalini maana alishagundua kuwa angeweza kuhatarisha maisha ya mtoto.aliamua kujiuzulu baada ya muda mfupi wa lile tukio alikuwa ameshafanya kazi kwa miezi kadhaa haukufika mwaka. Akaamua kuelekea jimbo la Lousiana.
MAISHA YA FRANK LOUSIANA AKIWA NI MWANASHERIA
Frank akiwa Lousiana siku moja alikutana na moja ya mademu aliowahi kuwagegeda miaka ya nyuma. Huyu dada alikuwa mfanyakazi wa kwenye ndege. Frank alimwambia yule dada kipindi kile kuwa alikuwa ni co-pilot yaani rubani msaidizi. sasa akwambia si hivyo tu ila pia alikuwa ni mwanasheria. Alisomea urubani na pia alikuwa Mwanasheria.frank akawa anaendelea kumgegeda yule mrembo kwa mara nyingine tena. anajilia tu kiulani. ukitaka kupata mademu wakali unatakiwa uwe mjanja mjanja.
Siku moja wapo kwenye party usiku wakila bata yule dada akamkutanisha na mwanasheria aliyekuwa akifanya kazi kwa mwanasheria mkuu pale jimboni. Yule jamaa akavutiwa na Frank sababu Frank alidai kuwa yeye alipata Degree yake ya Sheria toka Chuocha Harvard. Jamaa akaona hiki kichwa sana maana Harvard wanaosoma kule si watu wa mchezo mchezo.ni Vipanga hasa si Chuo cha vilaza hata kidogo. Jamaa akamwambia kuna nafasi katika ofisi ya Mwanasheria mkuu. Akamwambia ambacho alipaswa kufanya ni kupeleka tu transcript yake kwa ofisi ya mtihani na kuomba nafasi ya kufanya mtihani ili akifaulu aajiriwe kwa hiyo nafasi.
Hii ilikuwa changamoto ambayo ilimpa hamu pia ya kujaribu, akiamini nayo atashinda tu.baada ya kufanya maongezi na mwanasheria frank aliamua kwenda kutengeneza transcript bandia/fake kutoka chuo kikuu cha Harvard. Alifanya kwanza utafiti ni kozi gani zinafundishwa chuo cha Harvard.alikusanya kila ambacho kilihitajika kwa ajili ya kutengeneza mfano wa transcript hiyo. Aisee… mpaka amemaliza ile transcript ilikuwa kama original.yaani mle mle….ingawa hakuwa amewahi kuiona transcript halisi toka chuo cha sharia.ilionekana kuwa ni yenyewe kabisa na akaamua kwenda kujaribu.
Hatua iliyofuatia ilikuwa ni kufanya mtihani .hivyo frank akanza kujifunza sheria kwa week kadhaa kabla hajaenda kufanya mtihani.alipoona na mambo mengi tayari anayafahamu aliedna kujiandikisha kwa ajili ya kufanya mtihani.akawapa transcript yake ya magumashi. akaruhusiwa kufanya.Alichemsha…si unajua hakuwahi kusoma sheria katika maisha yake yote. Lakini alikuwa na advantage..ule mtihani uki fail unaweza tena kuja kufanya tena na tena.unaruhusiwa kurudia.hivyo akarudia tena na this time jamaa alipasua kinoma na akapewa leseni ya kufanya kazi kama mwanasheria.
Na hapo hapo akaomba kazi kwa mwanasheria mkuu wa hilo jimbo ikafanyika interview.akafanikiwa kuajiriwa kama legal assistant akiwa anafanya kazi kama upande wa corporate law.akawa mbali na marupurupu mengine analipwa mshahara wa usd 13,000 kwa mwaka miaka hiyo. Ulikuwa mshahara mkubwa sana. Jamaa alionesha kipaji cha ajabu sana cha utapeli na usanii katika historia hapa duniani.katika ile ofisi kulikuwa na mfanyakazi mwingine mpya aliajiriwa ambaye yeye alisoma Harvard kiukwel kweli. Jamaa akawa ana mghasi sana kwa kutaka kila mara wapige stories za chuo na kutaka kuzungumzia jamaa wengine ambao walisoma pale chuo wakamaliza mwaka huo.akaona hii sasa itakuwa issue jamaa asije akamuumbua bure. Akaamua kuachana na kazi yake hii ya uana sheria na kuamua kutafuta kazi nyingine.
Akaamua kurudia ile kazi yake ya kwanza.lakini safari hii akaamua kuwa anafanya kazi shirika la ndege la Trans World Airways(TWA) hivyo akajipatia sare,akatengeneza leseni mpya ya FAA,na kadi na kila kitu kilichotakiwa kama alivyofanya kule PanAm. Akaanza kupiga kazi tena akisafiri sehemu mbali mbali duniani na ku Cash bank mbalimbali ambazo kipindi kile hakuzigusa.
FRANK AKIWA UTAH (Profesa wa Sociology)
Jamaa katika pita pita yake akafika mpaka Jimbo la Utah hili jimbo lilimvutia kwa uzuri wake na pia kuw ana warembo wengi sana. Jamaa akenda mpaka maeneo ya kampasi za chuo...daah aliona watoto wakali sana.asikwambie mtu.udenda ulimtoka akajua hapo sasa inabidi kupiga kambi ili aweze kuwagegeda ipasavyo watoto warembo. Nia alikuwa nayo ,uwezo (pesa) alikuwa nao na sababu pia alikuwa nayo.
Jamaa akaomba kazi chuoni ili afundishe. Alipata akawa anawapiga pindi watoto warembo hapo chuoni.huku jioni anawapangia ratiba ya kuwagegeda.apewe nini na shetani?acha awachape watoto warembo.
Jamaa akaamua sasa ahame kile chuo akaombe chuo kingine kufundisha chuo cha Brigham Young University. Akafanya appointment akijifanya yeye ni Profesa wa Sociology. Akawa amewasiliana na Dean na kumwambia alifanya kazi ya kufundisha kwa miaka kadhaa kabla hajaacha na kuwa Rubani. Na akasisitiza sasa anataka kurudi katika kazi aliyokuwa akiipenda sana. Kazi ya ualimu. Yule dean alivutiwa sana na uzoefu mbalimbali aliokuwa nao frank na pia uchangamfu wake.
Akiwa na vyeti mbalimbali feki Frank akafanikiwa kupata interview na Dean akaamua kumwajiri akiwa amevutiwa naye sana. Akakubali kumpa ajira akiwa amepewa kozi moja aifundishe kwa semester nzima. Jamaa akaamua kwenda library kujiandaa kwa ajili ya kufundisha kozi hiyo. Hatimaye kwel akapewa mkataba wa kuajiriwa kwa semester moja awapige kipindi watoto wa kidosi akiwa kama Profesa Frank.alionekana kufurahia kazi hii mpya ingawa ilikuwa ni kwa muda tu maana hakuwa amepata mkataba mkubwa. Anapiga vipindi lakini pia anapata muda jioni wa kuwagegeda watoto wazuri ambao wanasoma pale chuoni na salary anapata kama kawa. Jamaa alikuwa anaua ndege wawili kwa jiwe moja.kazi na dawa. Kazi hii hakudumu nayo sana kwa kuwa dean alimtaka kuwa asubiri nafasi itokee ya kudumu kwa kuwa chuoni hawakutaka tena kuajiri walimu wa muda mfupi.
SAFARI YA KWENDA CALIFONIA.
Frank akaondoka zake Utah huku akiwa amejilia kiasi cha kutosha nanii za watoto wakali wabichi wa UTAH…akaamua kuelekea Califonia. (Unaukumbuka wimbo wa Tupac califonia Dream? Hili jimbo nalo lina maraha yake huko Marekani. Binafsi niliwahi fika huko kumekucha hasa) akiwa anaelekea huko akafikiria kurudia tena kazi yake ambaya huifanya vizuri zaid. Kuandika check za magumashi.kipindi hiki akawa amepata uzoefu mkubwa zaidi katika kipengele hiki. Aliweza kuandika check kubwa kubwa za maelfu Zaidi ya mara ya kwanza.aliweza kujikusanyia Zaidi ya USD 100,000 kwa kipindi hicho. Ukiziconvert kwa sasa zinakuwa nyingi Zaidi.
Alikuwa kijana mdpgo mwenye mkwanja wa kutosha kwa umri wake….alikuwa na ukwasi mwingi tu huyu bwana mdogo.bado alikuwa na upweke kiasi flani.maana kumbuka alikuwa ana vitambulisho mbalimbali.mara doctor,mara mwanasheria,mara profesa,mara…. Yaani ili mradi jamaa aliweza kuwa kila kitu.angeamua hata kufake kuwa yeye ni baba yako ungemwamini nakwambia.angekuja angekueleza yeye ndo baba yako kweli kweli huyo uliye naye siye..na angeweza hata kumshawishi mama yako…usiombee ukutane na frank mtaalam.jamaa alikuwa kichwa hasa.
Basi katika pita pita zake akafanikiwa kumpata mtoto mmoja mkali sana.wakapendana. huyo binti alikuwa ni mfanyakazi wa kwenye ndege. Na nikuambie kitu? Ukitaka watoto wakali sana… angalia wafanyakazi wa kwenye ndege,aisee ni wazuri sana..kama umepanda panda ndege wengi wao ni wazuri sana.sema yale maumbo yetu ya miss bantu huyapati.
SEHEMU YA MWISHO.
Basi frank akawa amempenda sana yule mtoto na alitamani kabisa kuwa waishi wote na katika kuzidiwa na mapenzi ye mwenyewe akaamua tu kumwambia ukweli yule binti.akajichana ye mwenyewe. Unajua hakuna kitu kigumu kama kukaa na siri…trust me ni ngumu sana yaani sometime unatamani hata uende porini ukaseme siri yako then baada ya hapo unajisikia kama umetua mzigo mkubwa.kama tu ile story ya mfalme aliyekuwa na masikio ya punda. Yeye aliamini kwa kumwambia huo ukweli basi yule mwanamke atamsamehe na kuyachukulia yale kama ni madhaifu yake na wakasonga mbele pamoja wakiishi real sasa.maana jamaa alikuwa hata hujui leo ye ni frank au john au abel....
Mshkaji alifanya kosa. Usiwaamini sana mademu… jamaa alitegemea kuwa demu angemwona amekuwa mwaminifu na sasa wasonge mbele kumbe sivyo.dem akaenda kumchoma FBI na kuwalezea alipo. bahati nzuri Jamaa wa machale alifanikiwa kuwatoroka akawa tena anaishi maisha ya kimachale machale. Jamaa akasafir mpaka ufaransa. Na akiwa katika ndege akakutana na demu mmoja mkali mfanya kazi wa kwenye ndege wakaanza mahusiano. Aligundua kuwa baba wa yule demu anamiliki duka la kuprint pictures na stationary. So akawa anatamani sana akutane na baba wa yule binti.kweli ikatokea akakutana na baba ya bint yule.frank akamwambia mzee kama atakuwa tayari kupiga naye kazi.yaani waprint kazi moja yenye mshiko kwa ajili ya PanAm.frank akamwambia mzee anampa tenda ya kuprint check 10,000 za payroll kwa wafanya kazi wa PanAm.yule mzee hakuwa na hiyana akaona mchongo si ndo huu. Akapiga kazi
Frank akazichukua hizo checks na kuanza kuzitumia katika Mabank kadhaa hapo hapo ufaransa.akajikusanyia makwaru kwaru (pesa) kibao. Halafu haraka sana akapanda mwewe kurudi USA ambako pia aliendelea kujikumbia mkwanja kwa njia zake haramu za kimazabe mazabe.
Muda si mrefu baada ya kurudi US. Siku moja Manjagu wakambananisha airport ya Boston akiwa anataka kupanda mwewe akale bata jimbo lingine. Jamaa wakamweka kwanza korokoroni ili waendelee kukusanya ushahidi mbalimbali kuthibitisha kama alikuwa ni yeye yule jamaa mtukutu sana Frank A.jr hata hivyo Manjagu /polisi walishindwa kupata kwa usahihi ushahidi wa kutosha yeye ni nani hasa. Walikuwa wamweka tu korokoroni hajapelekwa hasa segerea kwenyewe.ushahidi wa kutosha ukawa umekosekana na mwishowe akaachiwa kwa dhamana akiwa ameponea chupuchupu kuja kukamatwa na FBI ambaye alikuwa ametumwa kwenda kumtafuta. Jamaa ikawa kama wamempiga chura teke… si unajua humkomoi ukimpiga chura teke unamwongezea mwendo. Basi akazidi kuwa jasiri badala ya kukatishwa tamaa au kuingiwa woga.
Baada yu ya kutoka akaenda kuazima sare za walinzi au sercurity guard na kwenda kusimama pale pale uwanja wa ndege ambako mamwela walimkamata masaa kadhaa yaliyopita. Alikuwa ameshikiria mfuko mkubwa maalum ambao alikuwa anasubiria watu waweke deposits/pesa zao kila wanapokuwa wanapita au kusafiri kama ulivyo utaratibu. Wakawa hawana shaka wanaenda wanaandikisha zinahesabiwa wanakuja wanaweka kwenye ule mfuko/begi maalum alioshika frank wanaendelea na shughuli zao. Lile begi lilipoanza kujaa aliamua kulibeba kupeleka kwenye gari alilokuwa amekodi. Lilikuwa zito maana kulikuwa kumewekwa mapene kichele (pesa nyingi sana). Basi wale jamaa wengine wakaamua kumsaidia mshkaji pasipo kujua wanamsaidia mwizi katika mchakato wa kuondoka na pesa za wizi.jamaa siku ile ile moja tu alipiga zaidi ya usd 60,000 akaweka begani akalala nazo mbele.ilikuwa noma ile mbaya…. Polisi walikuja kumgwaya hapo baadaye si kwa usanii ule.
Kukamatwa
Frank akawa anaonekana ameshindikana karibia kwenye kila kitu alichokuwa akifanya.alifanikiwa kuwakwepa manjagu na hata FBI kwa kila mpango mpya.aliendelea kufikiria namna ambavyo ataendelea kupiga mkwanja mrefu. Akaja na wazo lingine.aliamua kuwa kwa sasa hatakuwa anasafiri peke yake. Atakuwa anasafiri na warembo kibao. hii itasaidia aweze kuwa ana cash mkwanja zaidi .maana unapokuwa umezungukwa na mademu watu hawakutilii shaka hata kidogo hivyo akaona aibuke na mbinu hi ya kutembea na watoto kadhaa wakali.
Akiwa anatembelea Arizona Frank akaweza kufanya mchakato wa kuoana na Director/Mkurugenzi aliyekuwa anahusika na masuala ya wanafunzi vijana katika vyuo vya serikali jimboni hapo.yaani kuwapeleka vyuo mbalimbali wanapoomba na pia kushughulika nao wanapomaliza kwa masuala ya ushauri na kazi. Akawa amaeongea naye uwezekanao wa kuajiri wanawake wengi kama maafisa uhusiano kwa ajili ya PanAm. Na akamwambia wanawake ambao atakuwa amewachagua watapata hata nafasi ya kwenda kutembelea Ulaya kipindi cha majira ya joto. zaidi zaidi hao wanawake watapewa mpaka uniforms au sare za PanAm,watapewa mshahara na barua za ajira pindi wamalizapo tu masomo yao.
Ilikuwa patashika pale chuoni watoto wazuri wengi waliomba hiyo nafasi… kila mtu alitamani awe mfanyakazi wa kwenye ndege..na si unajua watoto wakali wanapenda maisha yale ya kuzunguka tu na mwewe angani huku wakial bata sehemu mbalimbali duniani.katika kusagula sagula humo ndani akajipatia watoto nane wakaliiiiiii balaa.hawa walikuwa wakisisimkwa na vinyweleo kusimama wakiwaza jinsi ambavyo wataizunguka dunia ndani ya mwewe.halafu wakawa wanawaza pia jinsi ambavyo watakuwa wanalipwa kula bata. Just imagine unaenda kula bata na bado unalipwa pia.hawakujua.hawakujua.
Lengo la Frank lilikuwa kuwatumia hao mademu wakali kwenda ku cash zile check zake za kimagumashi hivyo akawa anaandika check za malipo makubwa kuliko hata ya kawaida. Akiwa huko huko bado alikuwa anawala kwa zamu tartiiiiibu.kama Analia vile.kwa hiyo muda wote akawa anazunguka nao wakiwa wamevaa zile sare wakifurahia sana na akawa anaenda nao bank ku cash zile pesa na huko hawakuweza kumtilia mashaka hata chembe maana unawezaje kumtilia mashaka mshkaji amezungukwa na watoto wakali wa kibongo,kilatino,kitasha n.k tena wamevaa sare za PanAm. Huwezi.kumbe jamaa anawapa tu za chembe kimya kimya anafinya mpunga wa kutosha kutokana na wao.inasadikiwa jamaa alikusanya mpunga wa zaidi ya usd 300,000 miaka hiyo. Si mchezo.
FRANK ANAHAMISHIA MASHAMBULIZI UFARANSA (MWANDISHI WA MOVIES ZA HOLLYWOOD)
Alipoona hii imefanikiwa akaamua tena apumzishe hii mbinu ili asije akashtukiwa. Akaamua kwenda Montpellier huko Ufaransa. Haikuwa mbali na alipokuwa amezaliwa mama yake. Akamua kutulia kwanza kwa muda kwenye nyumba tu ya wastani akiwa amebadilisha jina anaitwa Robert Monjo na akijifanya yeye ni mwandishi wa movies toka Hollywood.karibia mwaka hivi alijitahidi kuishi maisha ya kawaida tu.alikuwa amechoka sana na maisha ya kukimbia kimbia manjagu na FBI.
Siku za mwizi zilikuwa zinakaribia …na jamaa alishaacha hata kuzihesabu maana si unajua wanasema siku za mwizi ni arobaini?so kama unaiba hakikisha ukifika 39 unaacha. Jamaa mmoja mgwadu sana wa FBI alikuwa anaitwa Joseph Shea huyu alikuwa amekomaa ile mbaya kumtafuta Frank kwa miaka na miaka.maana FBI si kwamba walikuwa hawana taarifa zake.walikuwa nazo ila walikuwa bado hawampata ile bumper to bumper wanamlia tu timing. zaidi zaid ya kusikia tu mshkaji kapiga huku.wakienda hayupo,wanasikia tena kapiga bank flan wakienda hayupo. Jamaa alisema ye atakomaa naye tu mpaka kieleweke iwe mchana au usiku,iwe masika au kiangazi. Hakuna kulala.
Miezi kama minne hivi Frank akiwa France jamaa wa FBI alishapata taarifa hizo. Unajua ilichukua miaka mingi sana kufahamu kuwa Frank hakuwa mtu mzima ni bwana mdogo tu ambaye akili zimemzidia ameamua kuzitumia kihuni. Yule FBI alikutana na mmoja wa wafanyakazi wa ndege ambao frank alikuwa amewakamua. Akamwonesha picha kuwa anamtafuta jamaa.. yule demu akakiri anamfaham jamaa na kuwa yupo ufaransa sehemu flan ame chill tu.
Manjagu wa Ufaransa wakatonywa kuwa kuna mshkaji mmoja hafai ameshaziumiza banks mbalimbali Zaidi ya Usd 2.5 Million so yupo kitaani kwao wakamcheck. Wale wafaransa wakaona hii sasa issue yule mpigaji yupo nchini mwao.wakaanza mfuatilia na kuja kumkuta frank anafanya shopping mtaani kwenye kigrocery flani karibu na maskani mwake. Wakamdaka kumpeleka Montpellier Polce Station kumfungulia mashtaka kwa makosa aliyokuwa amewatendea pale ufaransa. Baada ya mahojiano frank alikuwabli kuwa yeye ni Frank A. Jr lakini akakataa kueleze kiundani makosa yake yote.hakutaka kuwapa habari yoyote kuhusiana na makosa yake. Ana bahati sana angekuwa ni mbongo halafu kakamatwa bongo akingepata kisago cha mbwa mwizi mpaka angeanza kuimba.
Ndani ya week frank akawa amepelekwa kwa pirato huko ufaransa na kukutwa na misala kibao..yaani alikutwa na madhambi au makosa mengi tu kwa mujibu wa sheria yakiwemo hayo ya utapeli. Wakampeleka kunyea debe segerea ya ufaransa kwa mwaka mmoja gereza moja la watu watukutu sana la Perpignan…. Aliishia tu kufungwa miezi sita. Ila hali ya mle ndani ilikuwa mbaya sana.wakamtoa.
Akapelekwa Sweden na baadaye Ufaransa. Huko akifanikiwa mara kadhaa kuwatoroka Manjagu na FBI na kuanza kuishi maisha ya kimachale machale… mwishowe akajikuta anasakwa ile mbaya.FBI wakamweka katika ile list yao ya wanted. Akajikuta hana pa kujificha na mwishowe alikuja kukamatwa akiwa amejificha huko New York si unajua mkono wa sheria ni mrefu sana. Na wale manjagu walishaona huyu jamaa si saizi yao wakampeleka kumkabidhi kwa wazee wa kazi wa FBI ( Female Body Intruder… ha haha am kidding bwana si maana hiyo) huko wakampeleka kwa pilato ili akapate stahiki zake kwa madhambi aliyowatendea wanagenzi mbalimbali.
Jamaa wakamhukumu kifungo cha miaka 12. Huko Virginia Gereza la Petersburg. Na hata hivyo akapata parole akiwa na miaka 26 akiwa ametumikia miaka 5 nyuma ya nyondo. Yaani alikuwa mpaka muda huo amechezea mvua 5 tu katika 12. Akaachiwa na kupata nafasi ya kuanza maisha mapya.
Baada ya kutoka segerea jamaa akaanza kuranda randa mtaani akitafuta vibarua. Ila life lilishakuwa gumu kinoma jamaa hakuzoea ku hustle namna ile na makashkash kibao akikimbizana na life.akawa anakamata kamata tu vijikazi kiasi vya kumtoa angalau asilale na njaa.alikuwa mara nyingi akijitahidi isijulikane kuwa alikuwa ni tapeli na alishawahi fungwa.lakini mwishowe waajiri wake wakawa wanakuja kufaham ukweli na kumfukuza.
Baada ya muda Frank akaanza kuwa frustrated … yaani kama kupagawa flani hivi kimawazo sababu alijua kabisa ana kipaji ambacho sehemu flan mtu anaweza akakihitaji. Hivyo akawa anawaza kutafuta mteja ambaye angekuwa interested na ujuzi wake na hivyo kufaidika nao. Hivyo akaamua kutafuta namna ya kujitangaza. Kwa kushangaza kabisa watu ambao wangefaidika naye walikuwa ni FBI. Hawa FBI ndiyo ambao wangeweza faidika na kipaji alichokuwa nacho. FBi walikuwa wanahitaji kufaham namna mbavyo wahaalifu wanatumia akili kufanya uhalifu wao ili waweze kuwakamata wahalifu hao. Frank akaanza kuwapa lecture bure.alijua pia kwa kutoa elimu hii alikuwa analipa kwa jamii aliyokuwa ameiumiza kwa utapeli wake.kabla ya muda mrefu kupita ikaja kazi ambayo ingeweza kumlipa elimu aliyokuwa nayo ikawa inahitajika sana na makampuni mengi duniani. Makampuni mengi yakagundua yanaweza kuokoa pesa nyingi mamilioni au mabillion kutoka kwa matapeli ikiwa watakuwa na mtaalam wa utapeli ambaye atawasaidia. Hivyo frank akawa ni mtu ambaye anatumika kwa ajili ya kuwapa taarifa muhimu za kuzuia matapeli.
Jamaa akawa anaitwa huku na kule akawaelekeze na wanampa mkwanja wa maana hasa. Na mpaka leo hii frank anaheshimika na makampuni mengi akiwa amefungua kampuni yake ya kutoa ushauri na kulingana na website yake ya www.abagnale.com frank amekuwa akienda kupiga lecture,akifanya consultation duniani nzima na kutoa semina na makongamano na vile vile akaamua FBI awe anawapa ushauri bure kabisa ingawa wao walikuwa wanataka wamwajiri.yeye aliona aitumikie FBI kwa nia hiyo ya kuwapa ushauri bure.
Jamaa ameandika vitabu vingi tu,Makala na mahapisho mbalimbali na ku design check ambazo ni salama zinazotumika na wafanyabiashara mbalimbali wakubwa duniani. Kiuhalisia hakuna shaka kabisa kuwa jamaa amekuwa akijitahidi sana kusahihisha makosa aliyoyafanya miaka ile ya nyuma na kipaji au akili yake kaipelekea katika mambo ya kujenga zaidi na si kuwapiga wenye makampuni na bank kama zamani na kula papuchi tu muda wote. Na jamaa ukimcheki amechange sana kwa sasa akiwa na mke ambaye wameishi naye Zaidi ya miaka 25 na kufanikiwa kupata watoto wa3. Jamaa amekuwa mtu wa dini sana kwa sasa. Anaenda church na kushirikiana na wadau wengine katika kujenga taifa. Ukimcheck kwa kweli ame change sana. Kwa sasa anaishi huko Midwest na mkewe na watoto wake vidume watatu.anakula kihalali. tuacheni uhalisi ndugu zanguni.....
Thursday, January 18
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment