Unapozungumzia simulizi za kusisimua kuhusu ulimwengu wa jela na wafungwa basi huwezi kumaliza na hakika utakuwa mtovu wa nidhamu kama utaacha kuweka kwenye orodha yako gereza tata na maarufu Nchini Marekani la Alcatraz!
Yes, Alcatraz nyumbani kwa watakifu wa uhalifu
Marekani miaka hiyo.
Gereza hili linapatikana katika jimbo la California kwenye ghuba ya San Fransisco katika kisiwa cha Alcatraz. Alcatraz lilifunguliwa rasmi mwaka 1934 baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa sana, na hadi mwaka 1935 tayari lilikuwa na wafungwa 242 kutoka maeneo tofauti tofauti na profile tofauti tofauti za kihalifu kabla ya kufungwa rasmi 21 March 1963!
Alcatraz lilikuwa chini ya idara ya magereza kitengo cha haki, na kabla ya hapo gereza hili lilikuwa Mali ya jeshi la Marekani kwa ajiri ya kuwatia adabu wanajeshi watukutu, na lilijengwa kwa Mara ya kwanza kati ya mwaka 1910- 1912.
*Kwanini Alcatraz?*
Gereza hili limekuwa maarufu sana na kupata utukukuzo kutokana na sababu kadha!!
1. Aina ya wahalifu waliopatikana hapo
2.Mazingira ya ulinzi na ya kijiografia kuzunguka gereza hilo
3.Mazingira na maisha ndani ya gereza.
Watukutu wa Alcatraz!!
Kama nilivosema hapo juu umaarufu wa gereza hili pamoja na mambo mengine unachangiwa na aina ya wahalifu waliopatikana humo. Hili ni gereza maalumu kwa ajiri ya watukufu katika ulimwengu wa uhalifu, hapa waliletwa watemi, walioshindikana katika mazingira yote ya Marekani, hapa wanakuja wale wenye 'shahada ya uzamivu' katika uhalifu, kuanzia wizi kwenye mabenki, mauaji, ubakaji, kulawiti, utekaji na wizi wa kutumia silaha.
Mwandishi mmoja analitaja gereza hili kama "the great garbage can of San Fransisco bay Bay, into which every federal prison dumped its most rotten apples" ( Alcatraz lilikuwa kama dampo kuu katika ghuba ya San Fransisco ambapo matunda( wafungwa)yaliyooza kuliko yote yalitupwa!"
Hii ni ndio Alcatraz!! Special to hold the worst of the criminals!
*Hawa ni watukufu wachache ndani ya Alcatraz.*
*1.Robert Franklin Stroud.*
Huyu alijulakana kwa nickname ya birdsman kutokana na kuwa mfugaji maarufu wa ndege nje ya shughuli yake tukufu ya uhalifu, alikaa Alcatraz tangy 1942 hadi 1959 na anatajwa kuwa mahalifu hatari kuwahi kutoka Marekani katika zama hizo!
*2.George Kelly (The Machine gun)*
Ni mtukufu mwingine aliyebahatika kutunukiwa tunu hii adhimu, ndani ya "the Alcatraz" alipewa jina la 'The machine gun' kutokana na mahaba yake kwenye chombo hiki cha moto wakati wa mission zake. Huyu jamaa aliongoza kundi wa wahalifu wa wizi wa mabenki na utekaji, kesi iliyompeleka Alcatraz ni kumteka mfanyabiashara Charles F. Urschek na kujipatia kiasi cha USD 200,0000.
3.Lakin pia anayeweza kuvikwa 'utukufu' zaidi wa Alcatraz ni Alivin Fransis Karps, huyu alikuwa kiongizi wa kundi lililojiita barber-Karpis, alikuwa Marekani mwenye asili ya Canada, anatajwa kama mmoja wa nguli wanne wa uhalifu waliopata kutunukiwa heshima ya kuitwa maadui wakuu wa taifa la Marekani miaka ya 1933 ambapo kati ya hao yeye pekee yake ndio alikamatwa akiwa hai, watukufu wengine walikufa kwa kipigwa risasi kabla ya kukamatwa, huyu jamaa ndio mfungwa aliyekaa miaka mingi katika utukufu wa Alcatraz… miaka 26 kati ya 29 ya uwepo wa Alcatraz!
*Ulinzi na mazingira kuzunguka Alcatraz*
Gereza hili lilikuwa na urefu wa kilomita 2.7, upana wa kilomita 1.5 na urefu wa mita 3.1 kwenda juu, huku likigawanywa katika blocks nne, block A, B, C na D, chumba cha Mkuu was Gereza, chumba ya wageni, Maktaba na Saluni ya kunyolea wafungwa, huku block "D" likiwa ndio block hatari zaidi kwa msoto kiasi kwamba pamoja na uhalifu wao katika uhalifu, watukutu hawa waliligwaya sana block hili!.
Gereza lilizungushiwa fence za umeme, electric detectors, radios na guard towers. Kikubwa zaidi ni kwamba gereza lilijengwa kwenye kisiwa kilichozungukwa na maji ya baridi mno panda zote na mkondo mkali sana!
Mazingira haya ndio yaliyolifanya gereza hili kuwa la kipekee na kuaminika kuwa gumu kuliko yote kwa mfungwa kutoroka! Hivyo kuonekana sahemu salama kabisa kwa watemi hawa kuishi, " Special to hold the worst of the Criminals"!
Maisha ya watemi ndani ya Alcatraz!
Waliopita Alcatraz wanakili haikuwa sehemu salama kwa kiumbe chochote cha mungu kuishi, lilikuwa na ukatili na maisha magumu sana, watemi walipata shuruba Kali kutoka kwa walinzi lakini wao kwa wao walfanyiana ukatili mkubwa mno. Edward Wulke ni mmoja wa wafungwa aliyekutana
na ukatili humo ndani, huyu jamaa alikatwaa mikono yake kwa shoka na baadae alikuja kujinyonga!
Mazingira walikuwa machafu mno kama inavyofahamika magerezani, kazi ngumu kwa muda mrefu huku likiwa ni kawaida sana kupitisha Siku tatu hadi nne bila kula huku wakiambulia slice mbili tatu!
Yote kwa yote block "D" ndio lilikuwa kiboko yao huku lilikuwa na selo zilizopatizwa shimoni, yaani ukiingizwa huku maji lazima uite mma! Hapa hapakuwa na umeme na kulikuwa na baridi Kali, huku wafungwa wakilazwa nusu uchi.
Lazima ukumbuke vitanda ni starehe iliyokuwaa hapitikani Alcatraz, vyoo vilikiwa si vya kiridhisha, watu walitembea peku peku, harufu mbaya ilikuwa nyumbani kwake!
Mmoja wa watu waliopata kuishi anakili kwamba Alcatraz ilikuwa ni kama jehanum na kama wangepewa nafasi ya kuchagua kuishi humo na kifo basi wangechagua kifo!
Kiufupi watukutu hawa walikuwa ni kama wafu walio hai, hadi hapo walikuwa na wazo moja tu, kutoroka! Au uendelee kuwa maiti inayoishi Alcatraz!
*Breaking the unbreakable!!*
Kwa mtu mwenye akili timamu ilikuwa haiwezekani kwake kufikiria kutoroka gereza la Alcatraz. Gereza lote lilikuwa ni kisiwa katikati ya bahari kilichozungukwa na maji panda zote.
Inasemekana ndani ya miaka 29 yalifanyika majaribio zaidi ya 14 yakihusisha watu 46, kati ya hapo wawili walikufa maji, sita walipigwa risasi, 23 walikamatwa na watatu hawajulikani walipo hadi sasa!
Mtu wa kwanza kujaribu aliitwa Joseph Bowers juhudi zake ziliishia mikononi kwa walinzi, walipigwa risasi baada ya kugoma kutii amri ya kujisalimisha!
Baaadae Theodore Cole na Raph Rae walikuja kufanikiwa kutoroka baada ya kukata nondo ya dirisha lakini wakafia majini kutokana na baridi kali!
*The battle of the Alcatraz!*
Hili jina lililopewa jaribio la kutoroka lilifanywa na watukutu sita, Bernard Coy, Joseph Cretzer, Sam Shockley, Clarence Carne's, Marvin Hubbard na Miran Thompson! Hawa baada ya kuwathibiti walinzi walifanikiwa kuingia chumba ya silaha na mpango ulikuwa watoroke kwa kutumia boti, lakini bahati mbaya wakakosa ufunguo wa boti! Hadi hapo mpango ukawa kama umegoma, Shockley, Thompson na Cornea wakaamua kurudi selo huku Bernard na wenzake wakiamua kuendelea na mission! Lakini hawakufika mbali kwani walipigwa risasi na wanajeshi wa Marines ambao walikuja kusaidia kutuliza varakangati hilo. Hapa walinzi wawili walipoteza maisha huku watu wengine saba wakijeruhiwa!
They didn't give up! It is not the end until it is end!
June 11 mwaka 1962 wanaume watatu, Frank Morris, John Anglin na Clearance Anglin wanafanikiwa kuvunja mwiko wa gereza hili wa wafungwa kushindwa kutoroka.
*Kulikuwa na siri gani nyuma ya pazia??*
Hawa jamaa walikuwa wakiishi kwenye sello ndani ya block "B" ambako pembeni ya sello yao lilikuwa na korido isiyolindwa, walichofanya ni kutoboa tundu kuunganisha selo yao na korido, shughulii ilifanywa kwa kutumia vijiko na drill walizochomoa kwenye mota ya cleaner, na walifanya kazi hiyo pindi unapopigwa mziki ili kuepuka kusikika wakichimba!
Baadae waliondoa feni kwenye roof, na kuweka nondo ambazo ziliacha uwazi wa kupita. Hapa walitumia faida ya korido kutokuwa na walinzi na kuwa sehemu yenye Giza! Inasemekana siku ya kutoroka walitengeneza vinyago na kujivika nywele kutoka salmon ( barber shop) na kuviweka sehemu wanazolala ili kuwapoteza maboya walinzi. Siku hiyo walimwamsha mwenzao Allen West,waliekuwa wamepanga mpango huu pamoja, lakini yeye akalala fofofo!
Baada ya tukio hili FBI walifanya upepelezi kwa muda wa miaka 7 hadi mwaka 1969 walipofunga kesi hii bila kuwa wameona miili ya hawa jamaa wala kujua walipo, wakaamua kuhitimisha kwamba jamaa walikufa maji!
Hapo hadi sasa kuna utata juu ya hilo, kwani wapo wanaodai jamaa hawa walifanikiwa kutoroka salama na wamekuwa wakiwasiliana na ndugu zao na kwamba walishawahi baadhi kuonekana Rio de Janeiro Brazil!!
0 comments:
Post a Comment