Ulimwengu (Universe) ni
mkubwa sana, yani mkubwa kupindukia na kila tunachoweza kuona kwa macho na pia
kwa technolojia ya juu kabisa, kama hizi telescope za Hubble, Chandra na
nyinginezo ni part ndogo tu ya ulimwengu na inaitwa “observable universe”. Size ya observable universe iliyokokotelewa na wanahisabati ni
kipenyo chenye urefu wa miaka bilioni 46 ya kusafiri kwa mwanga. Hii inaweza
kuelezewa hivi kama kuna nyota imelipuka leo katika kona ya mwisho ya upande
mmpja wa ulimwengu, baada ya miaka bilioni 46 kiumbe aliyeko katika sayari
upande wa pili wa ulimwengu ataona mlipuko huo. (hii ni iwapo mwanga huo
utaweza kufika). Hii inafanya galaxy yetu iwe kitu kidogo sana zaidi ya punje ya
vumbi ilivyo katika dunia.
Picha ya kufikirika ya kiumbe katika anga za mbali |
Ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana zinazofanana na jua letu
katika maeneo mengine ya mbali sana katika universe. Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na Jua
letu ni kati ya asilimia tano hadi ishirini (5% - 20%) ya nyota zote katika Universe tunayoweza
kuiona (observable universe). Hili neno la universe tunayoweza kuiona lina
maana kwamba pale tusipoona basi kuna uwezekano universe inaendelea au kunavitu
vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza
kuuona. Sasa ukumbuke katika mada ile ya Maajabu na Ukweli kuhusu Nyota za Angani, nilisema nyota zinakadiriwa kuwa sextillion 100
au zaidi katika ulimwengu tunaoweza kuuona sasa tukisema mfano tuchukue tu
asilimia 5 yake, basi tutakuwa tunaongelea nyota bilioni-bilioni 500 zinafanana
kimazingira (joto, ukubwa, umri, aina, uwepo wa sayari) na jua letu.
Sasa kwa number hizi basi ina maana uwezekano wa kuwepo sayari zenye maisha ni
mkubwa ingawa maisha yanaweza yasiwe haya tunayoyajua sisi. Utafiti wa
kisayansi uliyofanywa na PNAS (Proceedings of the National Academy of Sciences) unapendekeza kwamba kuna angalau asilimia moja
(1%) ya sayari zinazofanana sana na dunia yetu katika hizi nyota zinazofanana
na jua.
Wanaofikiri kuhusu dhana ya viumbe vingine nje ya sayari yetu hawatarajii sana
kuwepo na binadamu wanaofanana na sisi.Ingawa hilo linawezekana lakini kumbuka
kisayansi mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe. Kama
mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata
mkondo. Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi
wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Kwa kuwa hata
hizi sayari zinazofanana na dunia haziwezi kuwa na mfanano pacha yani
circumstance zile zile basi tusitegemee kukutana na viumbe wanaofanana asilimia
mia na sisi. Jinsi kila kitu kinavyoonekana leo hii ni matokeo ya jinsi
mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadri muda
unavyoenda.
Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na technology kubwa sana zaidi
yetu hili ni wazi na lina sababu zake. Kwanza kuna uwezekano wa utofauti wa
maisha kuanza hivyo kufanya viumbe wengine kama wapo basi wengine wanaweza kuwa
wame-evolve zaidi yetu kwa kuwa na muda mrefu zaidi katika ulimwengu. Kama
tukichukua mfano wa dunia yetu (Earth), maisha yanakadiriwa ku-evolve kutoka
katika simple form kati ya miaka bilioni 3.5 iliyopita hii ni kutoka kwa
evolutionists. Kuna sayari zilizo na muda mrefu zaidi ya dunia na hapa lazima
utaona katika hali ya kawaida sisi ndo tunaanza na kuna wengine waliokwisha
piga hatua kubwa sana. Na hata tukisema katika sayari nyingine kuna viumbe
waliumbwa au walitokea kabla yetu alafu sasa tujilinganishe nao lazima watakuwa
wametuzidi mbali.
Kama kuna kiumbe kikifika katika sayari yetu basi hii ina maana technology
inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Kuna umbali mrefu sana kati ya
nyota moja na nyingine hasa zile ambazo haziko katika mfumo wa nyota panya au nyota
kundi. Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa technolojia ya
usafiri tuliyonayo sasa. Mwendo wake ni miaka elfu sabini njiani kutoka hapa na kufikia nyota
jirani kwa speed kali kabisa ambayo space shuttle inaweza kwenda.
0 comments:
Post a Comment