Naibu
Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akisalimiana na wawakilishi wa
mashirika ya WHO na UNICEF alipowasili katika kambi ya maafa kuona
mazingira ya Kambi hiyo iliyopo Skuli ya Sekondari ya Mwanakwerekwe C
nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Naibu
Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akiongozwa na Afisa Msaidizi wa
kambi ya maafa Makame Khatib Makame kutembelea kambi hiyo iliopo Skuli
ya Mwanakwerekwe C.
Mwakilishi
wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmany Andemichael akiangalia dawa za Shirika la
Msalaba mwekundu alipofika Ofisi yao waliofungua kutoa huduma katika
kambi hiyo.
Afisa kutoka Shirika la WHO Zanzibar Michael Habtu akichunguza maji yanayotumika katika kambi ya maafa kujua ubora wake.
Naibu
Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji
Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar Ali Juma Hamad vidonge vya
waterguard na maji ya ORS kwa ajili kambi ya maafa, wa kwanza (kushoto)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum.
Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhi katika kambi ya maafa Mwanakwerekwe C.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Ramadhan Ali-Maelezo Zanzibar.
MAAFISA
wanaoshughulikia wananchi waliohifadhiwa katika kambi ya maafa
Mwanakwerekwe C wameshauriwa kutoa elimu ya Afya kwa wananchi hao ili
kuwaepusha na maradhi ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Naibu
Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman ametoa ushauri huo
alipoitembelea kambi ya maafa kuona mazingira na matatizo
yanayowakabili katika kambi hiyo akiambatana na wawakilishi wa Mashirika
ya WHO na UNICEF waliopo Zanzibar.
Amesema
kambi inakusanya watu wengi wenye desturi na taratibu za maisha
tofauti hivyo suala la kutoa elimu ya Afya itakayosaidia maambukizi ya
maradhi ni kitu muhimu .
Amewata
wananchi hao kufuata taratibu na maelekezo ya maafisa wa kambi hiyo
ikiwemo kunywa maji yaliyotiwa dawa na kukosha mikono baada ya kutoka
chooni na kabla ya kula ili wawe walimu wazuri watakaporejea kwenye
makaazi yao.
Afisa
Msaidizi wa Kambi ya maafa Makame Khatib Makame amemueleza Naibu Waziri
wa Afya kwamba hivi sasa kambi inawatu 420 wakiwemo wanawake 240.
Amesema
huduma zote muhimu zinatolewa ndani ya kambi hiyo na wameanzisha
utaratibu wa kuwapeleka na kuwarejesha watoto wanaosomo katika skuli
zao.
Wananchi
wanaohifadhiwa katika kambi ya maafa wameiomba Serikali kuweka
utaratibu wa kuwasaidia watakaporejea katika makaazi yao kwa vile
wamepoteza vifaa vingi vya matumizi baada ya nyumba zao kujaa maji.
0 comments:
Post a Comment