Thursday, March 31


Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
**
Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo kwa tuhuma za rushwa.

Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge wanatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa  ya shilingi Milioni 30 toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo 

Mwendesha Mashitaka wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mahela Ndimbo mbele Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,  Thomas Simba amesema tukio hilo lilitokea  Machi 15 mwaka huu  majira saa 2  had saa 4 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Ndimbo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa wajumbe Kamati Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) waliomba  rushwa ya sh.milioni 30 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana  Magota.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,Thomas Simba aliutakaupande wa mashitaka upeleke ushaidi  wa watuhumiwa wa rushwa .

Washitakiwa waliposomewa shitaka la kuomba rushwa wote walikana na dhamana yao kuwa wazi kwa masharti ya kila mmoja kwa na mdhamini wa mmoja wa sh.milioni tano pamoja na hati ya kusafiria ambapo wote walikidhi masharti ya dhamana hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ameairisha kesi hiyo mpaka Aprili 14 mwaka huu itakapotajwa tena .


0 comments:

-