Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utumbuaji wa majipu unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano haumuonei mtu, bali ni harakati za kupambana na wanaokwenda kinyume cha taratibu za nchi.
Akizungumza kwenye
mkutano wa wadau uliolenga kutoa taarifa ya hali ya kiuchumi na
maendeleo ya mikoa ya Katavi na Rukwa jana, Majaliwa alisema tangu
Serikali ianze kuwawajibisha watendaji wazembe kumekuwa kukizuka maneno
mbalimbali kwa baadhi ya watu wanaochukuliwa hatua hizo.
“Kaulimbiu
yetu ya ‘Hapa Kazi Tu’ inalenga kuwakumbusha wananchi wote kuwajibika
kwenye sekta zao ili kila mmoja azalishe na kutunisha pato la Taifa.
“Kipindi
cha kampeni tuliahidi kupambana na hali hii, ndicho tunachokifanya ili
kila mmoja atambue wajibu wake,” alisema Majaliwa.
Mkuu wa Mkoa
wa Katavi, Ibrahim Msengi aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Methew
Sodeyeka kwa nyakati tofauti, walisema bado wakazi wa maeneo hayo
wanakabiliwa na changamoto ya barabara.
0 comments:
Post a Comment