Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) pamoja na wafanyakazi
wa kampuni hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian
Maganga(watatu kulia) alipokuwa akiwafafanulia jambo juu ya studio ya
kurushia vipindi vinavyofanywa na kituo hicho, wakati wa ziara maalum
iliyofanywa na Uongozi wa kampuni hiyo kwa ajili ya mafunzo mbalimbali
na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kushoto) na Mkurugenzi
wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mtahaba (kulia) wakimsikiliza kwa
makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,( katikati )
alipokuwa akifafanua jambo juu ya utendaji mzuri wa kituo Clouds TV na
Clouds FM, wakati alipouongoza Uongozi wa kampuni hiyo kutembelea
makao makuu ya kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza
mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(kulia ) akimsikiliza
Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba(kushoto)
alipokuwa akimuelezea jinsi shughuli mbalimbali za utangazaji
zinavyoendeshwa na kituo hicho,wakati wa ziara maalumu iliyoongozwa na
Mkurugenzi huyo kutembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili
ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya
kibiashara.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akisisitiza jambo kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao( kushoto )
alipotembelea makao makuu ya kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa
ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya
kibiashara na kituo hicho,katikati Materi Mushi.
Mkuu
wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis
Sebo(kushoto)akiwafafanulia jambo juu ya studio ya kisasa ya EFM,
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kulia) na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn
Mworia (katikati) Wakati wa ziara maalum ya kujifunza mambo mbalimbali
na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo
Kawe jijini Dar es Salaam,kulia ni Mfanyakazi wa radio hiyo Kasampaida.
Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia, wakiwa katika
picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Redio ya EFM,Francis Ciza (Majey) baada
ya Uongozi wa Vodacom Tanzania kutembelea ofisi hizo kwa ajili ya
kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara
na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(katikati) Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn
Mworia(kushoto)wakioneshwa na Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio ya
EFM, Denis Sebo progaramu mbalimbali za
vipindi vinavyozalishwa na redio hiyo,wakati wa ziara maalum
iliyofanywa kituoni hapo na Uongozi wa Vodacom Tanzania kwa ajili ya
kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara
na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment