Watu wasiojulikana wamevamia katika makazi ya watu eneo la Msumbiji mjini Unguja na kuvunja mabanda na msikiti.
Watu
hao maarufu kama mazombi, walifanya uhalifu huo usiku wa kuamkia jana,
ambapo walivamia eneo hilo wakiwa wamejifunika nyuso zao na soksi
maalumu, huku wakiwa na silaha za jadi.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, amesema kuwa watu hao walivamia eneo hilo saa 10 alfajiri.
Alisema
watu hao baada ya kufika katika eneo hilo ambalo linadaiwa kukusanya
mashabiki wa vyama vya upinzani, walianza kuvunja mabanda ya mafundi
seremala.
“Lilikuwa
kundi la watu, tena wote ni mazombi, wakiwa na silaha za moto pamoja na
zile za kijadi kama mapanga, marungu, mikuki na mashoka.
“Wamefanya
uharibifu mkubwa wa mali zetu yakiwamo mabanda ya mbao, msikiti wa
mabati wa hapa Msumbiji ambao tumekuwa tukiutumia kama msikiti wa muda
wakati huu wa kisasa ukiendelea kujengwa.
“Vurugu
hizi wamefanya zimekuwa kubwa sana na uharibifu, huu kwa kweli ni
uonevu wa hali ya juu, wameharibu mabanda karibu yote kama unavyoona na
mengine ya biashara yaliyopo kando ya barabara hadi kufikia eneo la
mabati,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo .
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi lipo katika
uchunguzi.
“Tumepata
taarifa za tukio la kuvunja vibanda katika eneo la Msumbiji na Jeshi la
Polisi tumeanza msako wa kuwabaini watu waliohusika na tukio hili, ili
waweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema Kamanda Mukadam.
0 comments:
Post a Comment