Wanawake
wengi sana tumekuwa tukilia pindi tunapopata matatizo, tumeshindwa
kuvumilia yale yanayotupata, mfano hai ni mimi mwenyewe, hadi wengine
huniambia nina machozi ya promotion, hii pia nimeiona kwa wanawake
wengi, unalia weeeeeeee, ukinyamaza unaona kama umeshatua mzigo kwa
kiasi fulani, kama ni hasira basi unaona imepungua kwa sehemu,
utakuta
mtu anatafuta na private place, anajifungia kama ni chumbani peke yake,
analia kwa uchungu sana, na anaweza kuchukuwa muda mrefu sana kwa
kulia,
but problem inabaki pale pale
hali hii humfanya mwanamke kuwa mpweke sana kwa muda mrefu,
mwingine hataki kubembelezwa hata kidogo, yani ukimbembeleza ni kama umemwambia azidi kulia
Mwingine
akitoka kulia huwa na hasira sana, atapiga watoto, usimsemeshe, anaweza
kukupa jibu moja tu, ukanyanyua mikono juu. Lakini tatizo linakuwa
palepale, sasa hebu tusaidiane kushauriana juu ya hili, je inawezekana
mtu kuiacha hali hii??? na utaiachaje? ili ukipata tatizo usilie tena???
0 comments:
Post a Comment