Hatimaye
leo Bunge limeanza kujadili mpango wa maendeleo ya mwaka 2016/2017,
baada ya bunge hilo kutengua kanuni ili kupitisha mpango huo ambao
ulikataliwa wa baadhi ya wabunge wiki iliyopita.
Akiwasilisha
Mpango huo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema mpango
huo umeweka kipaumbe cha kuanzisha na kuendeleza viwanda vinavyotokana
na rasilimali zinazopatikana nchini pamoja na viwanda vya kuzalisha
bidhaa zinazotumiwa na watu wengi.
Dkt.
Mpango amesema katika mapango huo serikali imepanga kukusanya shilingi
trilioni 14.16 kutokana na mapato ya kodi katika mwaka wa fedha
2016/2017 ambayo ni ongezeko la asilimia 15 ikilinganishwa na mapato ya
kodi ya fedha yaliyokusanywa mwaka uliopita.
Aidha katika mwaka wa fedha 2016/2017, serikali imepanga kutumia shilingi trilioni 22 .99 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo ambapo kati ya hizo trilioni
16.80 itakuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni
6.18 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Amesema kati ya trilion 16.80 za matumizi ya kawaida, shilingi trilion 6.65 zitakuwa ni kwa ajili ya mishahara.
Aidha
amesema kuwa kati ya trilion 6.18 za miradi ya maendeleo, takriban
trilion 4 sawa na asilimia 77.8 zitakuwa ni fedha za ndani.
Bunge litakaa kama kamati kujadili na kutoka mapendekezo kwa ajili ya kuboresha mpango huo kwa siku tano kuanzia leo.
Mpango
huo uliingia dosari wiki iliyopita baada ya wabunge wa upinzani kukataa
kuujadili kwa madai kuwa serikali ilikiuka kanuni na taratibu za
kuuwasilisha bungeni.
0 comments:
Post a Comment