Thursday, January 14

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ni mmoja wa Marais wa Afrika ambao sio wageni kuingia kwenye headlines ya stori za utani hivi… karudi tena, alikuwa kwenye kikao na waandishi wa habari Uganda, kwenye stori zake akagusia na imani yake kwenda mbinguni.
Kaja na sentensi hizi hapa >>> “Nina malengo serious kabisa ya kwenda mbinguni, kama nyie mna mpango wa kwenda kuzimu kazi kwenu… Ila kwa mimi nina dhamira ya wazi kabisa kuiona mbinguni.”- Rais Museveni.
MUSEVENI II
Rais Yoweri Museveni akisoma biblia.
Sentensi nyingine hizi hapa, Rais Museveni kamaanisha hatanii kwenye hili >>> “Haiwezekani nikafanya mengi, nikatoa sadaka vya kutosha duniani alafu nifike huko niambiwe niende kuzimu…

0 comments:

-