Na Raymond Mushumbusi Maelezo
Rais
mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa
Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa mahusiano ya kimataifa Leo
Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Mhe.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa shahada
hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao
wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao
kiutendaji.
“Naipokea
heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona
mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na
ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt Kikwete.
Mbali
na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali
duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria
Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais
wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya
Kusini Hayati Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa
UNESCO.
Chuo
kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada
maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya
uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada
wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.
Tangu
kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania mwaka 1992 jumla ya wahitimu
25,908 wametunukiwa Shahada mbalimbali na haya ni mahafali ya 30 tangu
chuo kuanzishwa.
Rais
mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ( Kulia)
akifatilia kitabu cha mahafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania
yaliyofanyika Jijini leo Dar es Salaam. kushoto ni Prof Suh Chae-Hong
Rais wa Chuo cha Chosun kilichopo Korea ya Kusini..
Maandamano ya wanataaluma katika Mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akifungua rasmi
mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar
es Salaam.
Mkuu
wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimtunuku Shahada ya
ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa Rais mstaafu
wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika maafali ya 30 ya
Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimpongeza Rais
mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku
Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa
katika mahafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo
Jijini Dare s Salaam.
Rais
mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na
wanataaluma na wageni katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania
yaliyofanyika leo Jijini Dare s Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali kutoka Chuo kikuu Huria Tanzania.
0 comments:
Post a Comment