Kukabiliana na uhalifu mtandao lazima papatikane mashirikiano "Collaboration"
– Mashirikiano ya ndani pamoja na nje. Mara baada ya Hotuba yangu
Nchini Afrika kusini ambapo niliibua dhana ya kuwekea mkazo kwenye
kuimarisha ushirikiano kwani uhalifu mtandao hauna mipaka na uharibfu
wake ni wa kupindukia. Mengi yameendelea kuonekana na dhana imeendelea
kubeba uzito huku mataifa mengi yakihakiki yanazingatia hili kwa
kuanzisha au kuunganisha vitengo vinavyosimamia dhana ya ushirikiano.
Aidha,
Bado uhalifu mtandao umeendelea kukua maeneo mbali mbali ambapo
imeonekana wahalifu mtandao wamejipanga upya na nguvu mpya – Huwenda ni
baada ya Raisi wa Marekani Kuzuia kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka
jana kukutana. Hatua aliyoichukua baada ya kuona mikutano yao ya
kihalifu mtandao ilikua ikionyesha mafanikio kwa kukuza uhalifu mtandao
maeneo mengi duniani hata Taifa hilo.
Tahadhari
na maangalizo mbali mbali yameendelea kutolewa ili kuruhusu makampuni
,watu binafsi na Mataifa kujipanga zaidi na dhana ya kuzuia tatizo kabla
halijatokea. Ambapo katika hotuba yangu Nchini Kenya mwishoni mwa mwaka
jana hili nililiimiza zaidi.
Kama
ilivyo ada, katika kupitia mapitio kadhaa ya kihalifu mitandao na
ukuaji wa matumizi ya TeknoHAMA tumeendelea kutoa taarifa ya mategemeo
ya uhalifu mtandao katika mwaka huu ili pia kutoa fursa ya mataifa
kujipanga kukabiliana nayo yatakapo jiri na hata kujitahidi kutengeneza
njia rafiki ya kuzuia kabla hayajatokea.
MAFANIKIO
Mapema
mwanzoni mwa mwaka huu hatimae wahusika wa uhalifu mtandao uliotikisa
anga ya usalama mtandao ambapo pesa nyingi zilifanikiwa kuingia mikononi
mwa wahalifu baada ya kufanikiwa kuingiza kirusi cha Tyupkin kwenye
Mashine za kutolea fedha "ATM" na kusababisha pesa kutoka bila mpangilio
wamefanikiwa kutiwa nguvuni. Taarifa ya Tyupkin ilipojiri niliitolea ufafanuzi kupitia andiko linalosomeka kwa “KUBOFYA HAPA”
Aidha,
Kupitia dhana ya ushirikiano baina ya mataifa mbali mbali ambapo pia
imekua chanzo cha kufanikisha upatikanaji wa wahusika wa Tyupkin,
Watuhumiwa wengine wa wili waliohusika na kundi la “DD4BC DDOS
extortion” wametiwa nguvuni.
Mpango
kabambe ulipangwa kuhakiki kundi hili lililo umiza vichwa vya
wanausalama mitandao linasambaratishwa ambapo mataifa mengi
yaliunganisha nguvu kukabiliana nalo na hatimae wiki hii mwanzoni ndoto
ikatimia. Inaaminika wawili waliotiwa nguvuni si mwisho wa tatizo na
bado jitihada zaidi zinaendelea.
KASI YA UHALIFU MTANDAO
Wakati
mafanikio kadhaa kutoka katika mataifa mbali mbali hasa barani Ulaya
ambapo kwa hakika tayari wamekua na mpango madhubuti baina ya Nchi zao
kukabiliana na uhalifu mtandao huku wakishirikiana kwa karibu na mataifa
nje ya umoja wao kufikia malengo bado tumeendelea kuona matukio kadha
ya kihalifu mtandao ndani ya mwaka huu katika maeneo mengi.
Nchi
ya Ukraine, Wahalifu mtandao walifanikiwa kuzima umeme ambapo tukio
hilo limetafsiria kama “Wakeup call” kwa mataifa mengine kwani tayari
hili lilisha bashiriwa kua mataifa yajipange kwenye mifumo ya umeme
kwani wahalifu walisha tengeneza mikakati ya kuidukua na kuleta madhara.
Taarifa
za awali zinaeleza kua uhalifu huo chanzo kimeonekana kutokea Nchini
Urusi. Marekani imeshasema itatoa ushirikiano wa dhati kujua mzizi wa
tukio husika na ufumbuzi kupatikana. Wakati Marekani ikijipanga kutoa
usaidizi kwenye hili- onyo limetoka kua huwenda nayo ikawa nchi
itakayofatia kwenye uhalifu huu hivyo nayo ijiweke/ijipange vizuri
mapema.
Nissan
nayo haijabaki salama, Wahalifu mtandao wa kundi la “Anonymous”
wamefanikiwa kuidukua na kuiangusha wakidai ni namna yao ya kuandamana
dhidi ya Japan. Nissan kufuatia tukio hilo ililazimika kufunga tovuti
zake mara moja ikiwa ni hatua za kuhimili vishindo vya uhalifu huu
mtandao dhidi yake.
Swala
la Makampuni ya magari kudukuliwa sio geni na mwaka jana tulishuhudia
magari aina ya "Jeep" kuingiliwa na wahalifu mtandao yaliyosababisha
magari hayo kupata ajali zisizotegemewa baada ya wahalifu mtandao wakiwa
mbali kuweza kuyasababishia ajali hizo.
Nigeria
pia Hamkani si shwari , Jumatatu ya wikii hii, Wakati ufunguzi wa
mafunzo maalum ya kiuslama mtandao – Waziri wa TEHAMA wa Nchi hiyo Mh.
Adebayo Shittu aliainisha kupitia hutuba yake kua makundi ya kihalifu
mtandao yameendelea kulitesa taifa hilo kwa kuathiri wizara, mashirika
ya kiserikali, mashirika ya kifedha na penginepo ambapo uhalifu huo
umeendelea kuigharimu nchi hiyo zaidi ya dola za kimarekani Milioni
400 kila mwaka.
Mafunzo
hayo maalum ni katika utekelezaji wa azimio la kuongezea uwezo wataalam
tulio nao – Azimio ambalo limeendelea kutekelezwa na mataifa kadhaa
kitaifa. Binafsi nategemewa kuendelea kushiriki kwenye mpango huu kwa
Nchi ya Kenya kufuatia mwaliko maalum. Nitumie fursa hii kutoa wito kwa
taifa la Tanzania kuliangazia hili kwani ni moja ya njia sahihi za
kukabiliana na uhalifu mtandao nchini.
Marekani
nako wahalifu wame chachamaa, Nchi hiyo imetoa tamko kua kufuatia
uangalizi kwenye mitandao yake, imebaini wahalifu mtandao waki vamia
zaidi mifumo ya makampuni yao na tayari wameaza kuimarisha namna ya
kukabiliana na uvamizi huo huku ikitahadharisha kuonekana kwa uhalifu
mtandao kutegemewa kutatikisa zaidi mataifa mengi mwaka huu.
ANGALIZO - TAHADHARI
Microsoft
imetangaza kwamba imeacha kutoa usaidizi wa kiufundi kwa matoleo ya
awali ya kisakuzi chake cha Internet Explorer na kuwaweka hatarini
mamilioni ya watu wanaotumia matoleo hayo.
Mabadiliko hayo yataathiri matoleo nambari 8, 9 na 10 ya kisakuzi hicho.
Baadhi
ya mashirika yanakadiria kwamba matoleo hayo hutumiwa na takribani
asilimia 20 ya Computerworld inasema kati ya watu wanaotumia Internet
Explorer, ni asilimia 55 pekee wanatumia matoleo ya majuzi zaidi.
Visakuzi
hulengwa na wadukuzi na wataalamu hubashiri uwezekano wa mashambulio
kutokea na kuweka kinga kupitia kutoa matoleo mapya.
"Kuanzia
Januari 12, 2016, ni toleo la karibuni zaidi la Internet Explorer
litapokea usaidizi wa kiufundi na maboresho ya kiusalama,” Microsoft
wamesema.
"Microsoft inawahimiza wateja kuboresha na kutumia toleo la majuzi zaidi na ili kuchakura mtandaoni kwa njia salama zaidi.”
Kampuni hiyo inaendelea kutoa usaidizi kwa matoleo ya IE 11 na Edge, ambayo kimsingi ndiyo hutumiwa na Windows 10.
NetMarketShare
inakadiria kwamba wanaotumia Internet Explorer mtandaoni ni 57%
wakilinganishwa na 25% wanaotumia Chrome, 12% wanaotumia Firefox na 5%
wanaotumia Safari.
Aidha,
Uhalifu unao sababisha kufunga kwa mfumo wa mtumiaji na kumtaka atoe
kiasi cha pesa ili aweze kuendelea na huduma maarufu kama “Ramsomware”
unashika kasi hivyo makampuni na watu binafsi hawanabudi kujipanga.
MATARAJIO 2016 YA KIHALIFU MTANDAO
Watu
binafsi, Makampuni na mataifa yameaswa kujipanga zaidi kufuatia
matarajio na ongezeko la uhalifu mtandao mwaka huu ambapo zaidi
tunategemea kuona na baadhi tayari yameanza kuonekana uhalifu mtandao
utatikisa zaidi maeneo yafuatayo.
Matarajio
ni kua Sekta ya Umeme, Anga na Elimu (Vyuo) vitegemee kupata itilafu ya
kiuhalifu mtandao. Bado Mabenki nayo kupitia aina tofauti kadhaa mpya
za uhalifu ili kuiba pesa ni miongoni mwa vinavyo tajwa.
Sekta
ya Umeme tayari tumeona Ukraine ikifungua dimba huku mataifa mengi
yakiaswa kujipanga. Wakati huo huo sekta ya Anga mpango kabambe wa
kuimarisha kujipanga umewekwa huku tamthilia ya “CSI Cyber” ikitoa
episodi maalum kulizungumzia hili mapema mwaka huu.
Hili
likijiri Umoja wan chi za Ulaya “EU” imeanzisha rasmi “Digital ‘SWAT’
Team for Aviation” ambapo wataalam wabobezi watapata ajira kukabiliana
na kujipanga dhidi ya tishio hili la kihalifu katka sekta ya Anga.
Vyo Kadhaa tayari vimeingiliwa na wahalifu mtandao na baadhi wametiwa nguvuni huku mataifa kadhaa yakijipanga kwenye hili.
Matarajio
haya ni kwa uchache – Ila jitihada za mwaka huu maangalizo na kutumia
njia mbali mbali patakua na mpango kabambe ya kuyatolea ufafanuzi
sanjari na kuainisha namna ya kujipanga kukabiliana na hali mbaya ya
kihalifu mtandao.
Nichukue
Fursa hii tena kutoa wito kwa taifa la Tanzania kua sikivu kwenye hili
ili kuweza kujipanga mapema na hali ya kihalifu mtandao kabla ya mambo
kuharibika na kuanza kukimbizana kutafuta suluhu ya changamoto.
0 comments:
Post a Comment