Stori: Musa Mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Kimenuka mbaya! Gumzo kubwa mjini ni timbwili ‘hevi’ aliloliangusha Mbongo-Fleva wa kike, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au Shishi’ ndani ya Studio za Clouds TV mara tu baada ya kumuona aliyekuwa mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ katika zoezi la kutaka kuwapatanisha baada ya kutemana hivi karibuni hivyo mahojiano yakavurugika na kwamba upatanisho haukufanikiwa.

Mara tu baada ya kuchomoka kwenye
‘intavyu’ hiyo, Shilole alitimkia nchini Afrika Kusini (Sauz) lakini
alipata nafasi ya kuzungumza na gazeti hili kuelezea kile kilichotokea.
Shilole alisema, hakuna siku amewahi
kufikia wakati mgumu kama siku hiyo ambapo aliitwa na mmoja wa
watangazaji wa Clouds TV, akimuomba wafanye mahojiano na akakubali
akijua yatakuwa ni mahojiano ya kawaida yahusuyo muziki na shughuli zake
zingine kama msanii wa kawaida.
Alisema kuwa kwa upande wake intavyu
hiyo ilikuwa ngumu mno kwani hakutarajia na maswali yaliyomhusu Nuh
Mziwanda ndiyo maana yakatokea yaliyotokea.
“Ile kugonga vitu na kutaka kutoka
ilikuwa ni hasira kwani nilikwazika sana, ningejua mapema kuwa wameniita
kukutanishwa na huyo Nuh kweli nisingeenda,” alisema Shish
0 comments:
Post a Comment