Wednesday, November 11


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UCHAGUZI WA UBUNGE NA UDIWANI ULIOAHIRISHWA KUTOKANA NA VIFO VYA WAGOMBEA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa Ubunge na Udiwani katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi tarehe 25 Octoba 2015 kwa sababu za vifo vya wagombea sasa Uchaguzi huu utafanyika tarehe22 Novemba 2015; 13 Desemba, 2015 na 20 Desemba, 2015.

Majimbo,Kata na tarehe watazofanya Uchaguzi ni kama ifuatavyo:

22 Novemba 2015
Na.
JIMBO
MKOA
1.
LUSHOTO
TANGA
2.
ULANGA MASHARIKI
MOROGORO

22 Novemba 2015
Na
KATA
HALMASHAURI
1.
MULEBA
MULEBA KUSINI
2.
UYOLE
MBEYA MJINI
3.
BUKENE
SHINYANGA
4.
MSINGI
MKALAMA
5.
BOMANG’OMBE
HAI
7.
KASULO
NGARA DC
8.
BUKENE
SHINYANGA DC



13 Desemba 2015
Na.
JIMBO
MKOA
1.
ARUSHA MJINI
ARUSHA
2.
HANDENI MJINI
TANGA

13Desemba 2015
Na
KATA
HALMASHAURI
1.
MVOMERO
MVOMERO DC

20 Desemba 2015
Na.
JIMBO
MKOA
1.
LUDEWA
NJOMBE
2.
MASASI MJINI
MTWARA

-          Vituo vya kupigia Kura ni vile vilivyotumika wakati wa upigaji Kura za Urais Oktoba 25, 2015
-          Vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
-          Wanaoruhusiwa kupiga Kura ni wale walio na kadi za Mpiga Kura na wamo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

IMETOLEWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


Kailima,R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

0 comments:

-