Monday, November 2


Rihanna.
LOS ANGELES, Marekani
Diva anayetajwa kuwa miongoni mwa wasanii wa kike wakali kutoka Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’, amekula dili jipya la kusaini mkataba utakaodumu kwa muda wa miezi saba na Kampuni ya Simu ya Samsung ambapo itamfanya aingize kibindoni dola milioni 25 (sawa na zaidi ya Sh bilioni 50) atakazozitumia kugharamia ‘tour’ yake na kusapoti albamu yake mpya ya Anti.

Menejimenti inayosimamia kazi za Rihanna ya Roc Nation ambayo ipo chini ya Jay Z pamoja na meneja wake, Jay Brown iliridhia kusaini mkataba huo na kwa pamoja walisaidiana kukamilisha dili hilo kwa niaba ya Rihanna.

“Samsung inataka Rihanna awasaidie kupromoti simu yao aina ya Galaxy kupitia kazi yake ya muziki. Lakini hata hivyo bado tarehe rasmi ya kuachiwa kwa albamu hiyo haijapangwa licha ya kuwa ‘cover’ tayari imetoka lakini imerudishwa ili kufanyiwa marekebisho baada ya kupata dili hili,” ilisema taarifa kutoka Roc Nation.

0 comments:

-