Friday, November 27

Idadi ya makontena 31 yaliyobeba magogo yamekamatwa katika bandari ya Dar es salaam yakidaiwa kutokea Zambia.
Wizara ya Maliasili na Utalii baada ya kupata taarifa hiyo kupitia vyombo vyake vya upepelezi iliamua kufuatilia na kugundua makontena hayo yenye thamani ya zaidi ya milioni 300 yameingizwa nchini kinyemela na makampuni matatu ambayo bado yanafanyiwa uchunguzi.

DSC_1608
Baadhi ya magogo yaliyokamatwa
Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na utaliii Dkt.Adelhelm Meru amesema “Tulikuja na Balozi wa Zambia katika bandari hii lakini hatukuweza ku0na nyaraka yoyote inayoonyesha yametoka Zambia, tukajiuliza yametoka wapi? tulichobaini ni kwamba kuna watu waovu wachache ambao hufanya uhalifu na kwenda kukata maliasili zetu na kwenda katika mpaka wa Tunduma na kujifanya si mali ya Watanzania”..
Ameongeza kuwa “Kuna uwezekano mkubwa kuna watu wanakata magogo Mikoa ya Mbeya, Ruvuma na kuyapeleka hadi Mipakani na kujifanya yametoka katika nchi za jirani..hawa watu tutawashughulikia kwa kufuata sheria, wale wanaofanya uhalifu wa namna hii hatutawaacha hivi hivi wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria za nchi”….
DSC_1586
Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na utaliii Dkt.Adelhelm Meru akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa bandarini
“Makontena yaliyokamata yana gharama zaidi ya shilingi Milioni 300 na hatujui ni mangapi yameshapita na kusafirishwa kwa madai kwamba yanatoka Zambia, tumebaini ni makampuni matatu ambayo yamehusishwa katika uhalifu huu wa kusafirisha haya magogo”….
Balozi wa Zambia Elizabeth Phiri amesema “Ni kweli tumepokea ripoti ya magogo hayo ambayo yanasemekana yametoka Zambia lakini nchini kwao hakuna utaratibu wa kutoa kibali cha kusafirisha magogo zaidi ya kusafirisha mbao peke yao, kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kujua kiini cha magogo hayo yalipotoka wakishirikiana na Serikali ya Tanzania

0 comments:

-