TIMBWILI!
Njemba mmoja mkazi wa Kisimani mjini Tunduma wilayani Momba, Mbeya
ambaye jina lake halikupatikana mara moja, amejikuta akila kichapo kisa,
kudaiwa kumtorosha msichana wa kazi ‘hausigeli’ wa mtu. Tukio
hilo lililokusanya watu kibao, lilijiri juzikati katika maeneo hayo
baada ya vijana hao kumtuhumu kijana huyo kwamba amemficha msichana huyo
ambaye bosi wake aitwaye Johnson alikuwa akimtafuta. Wakizungumza na Amani
kuhusu tukio hilo, mashuhuda walisema vijana hao walipofika kwa
mtuhumiwa huyo walimtaka aoneshe alipo hausigeli huyo ambaye ilisadikiwa
kuwa yeye ndiye alikuwa naye. “Wale
vijana walisema walipeleleza na kubaini kwamba, msichana huyo wa kazi
yupo naye kwa sababu amekuwa akionekana naye mara kwa mara na kuna watu
wanaamini kwamba anatokanaye kimapenzi. “Mtuhumiwa
aliposema hajui alipo msichana huyo ukatokea ugomvi mkubwa, wakimshika
ili wampeleke Kituo cha Polisi Tunduma lakini walitokea watu wenye
kutaka amani wakamtorosha mlalamikiwa huyo kwenda kumficha mahali
kusikojulikana,” kilisema chanzo. Mtu
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Lupasyo Kingdom aliyedai anazijua
sheria ya Tanzania, alisema: “Kwa utaratibu wa sheria ilibidi wao waende
polisi kutoa taarifa za kupotelewa na msichana wa kazi halafu polisi
ndiyo waanze kumtafuta na si wao kuchukua jukumu la kutaka kumburuza
polisi mtu wanayedhani anahusika.”
0 comments:
Post a Comment