Monday, August 10

kt
Ukiachia soka, mchezo wa ngumi na tennis nayo pia iko kwenye list ya kupendwa zaidi na watu hasa kwa nchi za Magharibi.
Kwa upande wa mchezo wa Tennis nao umejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na mashabiki wengi na hata wachezaji kujikuta wakitajirika kupitia mchezo huo kama ilivyo kwa soka na masumbwi.
Leo nimekuletea list ya mastaa wa tenisi wanaoongoza kwa kuwa na utajiri zaidi duniani.
FEDER
1. Roger Federer ndiye mcheza tenis anaongoza kwa utajiri zaidi duniani ikiwa ni wa dola milioni 320 pamoja na kuingia mkataba wa dola milioni 52 na makampuni ya Nike,Rolex, Wilson
ANDRE
2. Andre Agassi amezaliwa katika mji wa Nevada USA, anashika nafasi ya pili kwa utajiri akiwa na dola milioni 175
PETE
3. Pete Sampras, amezaliwa Maryland USA, anashika nafasi ya tatu kwa utajiri duniani akiwa na dola milioni 150
SERENA4
4. Serena Williams, amezaliwa Michigan USA, na anakamata nafasi ya nne kwa utajiri akiwa na dola milioni 140, pia ameingia mkataba wa dola milioni 40 na kampuni ya Nike  na Kraft Foods
NOVAK
5. Novak Djokovic amezaliwa katika mji wa Belgrade, Serbia, anautajiri wa dola milioni 120
MARIA
6. Maria Sharapova amezaliwa katika mji wa Nyagan Russia, utajiri wake ni dola milioni 110
RAFAEL
7. Rafael Nadal amezaliwa katika mji wa Manacor Spain, ana utajiri wa dola milioni 100
VENUS
8. Venus Williams amezaliwa California USA, ana utajiri wa dola milioni 75
ANDY
9. Andy Murray amezaliwa katika mji wa Glasgow, UK..ana utajiri wa dola milioni 70
ANNA10
10. Anna Kournikova amezaliwa Moscow, Russia, ana utajiri wa dola milioni 50

0 comments:

-