Kikao cha Halmashauri Kuu kimeendelea
sasa hivi kwa zaidi ya saa nne hapa Makao Makuu ya CCM Dodoma, viko vitu
vingi vinaendelea nje ya Ukumbi… wapo wanaoimba na kushangilia,
wengine wapo wakiendelea kusubiri kile kitakachotangazwa baada ya
Halmashauri Kuu kumaliza Kikao.
Watu ni wengi sana nje ya Ukumbi,
nimebahatika kukutana na wenyeji wa Mji wa Dodoma na watu ambao
wanafanya shughuli zao kwenye Majengo yanayozunguka Makao Makuu hayo,
wanasema haikuwahi kutokea mtaa huu ukawa busy watu wakawa wengi kiasi
hiki.
Hapa ni nje ya Ukumbi ambao Kikao kinaendelea.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa nje ya Ukumbi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa nje ya Ukumbi pia.
Waziri Lukuvi akitembea kuelekea Ukumbini.
Hawa ilikuwa bahati mbaya wakapata ajali jirani na gari la Polisi.
Huyu alionekana kwenye vurugu nje ya Ukumbi, Polisi wakamchukua.
Gari nyingi za Polisi na FFU zimezunguka Ukumbi kuhakikisha Usalama upo wakati wote.
Wanaoshangilia hawajachagua pa kukaa, ni mchana jua kali lakini wapo hapa wakati wote.
Kila mtu kaaangalia panapomfaa, wengine wako juu ya ukuta.
Akina mama na wadada nao hawajaogopa kusimama juu ya ukuta.
Ripoti zote toka DODOMA utaendelea kuzipata hapahapa mtu wa nguvu,
0 comments:
Post a Comment