Monday, July 27

dunia
Vitendo vya Ugaidi ni miongoni mwa stori zinazoshika na kuweka headlines kubwa sana duniani, na kwa sehemu nyingi za dunia vitendo hivi sio vya mchezo kabisa.
Kutokana na ukuaji mkubwa wa vitendo ya Ugaidi duniani, makosa kama uwizi kwa kutumia mitandao, uhalifu wa IT na migogoro baina ya mipaka ya nchi ni vitu vikubwa sana, unaweza kusema hakuna nchi iliyo salama kabisa.
dunia4
Nimekutana na orodha moja iliyo orodhesha Miji 10 ya hatari duniani, Miji 4 ya Afrika imetajwa, ungependa kuijuwa? Nimekusogezea picha zake hapa chini.

1. Afghanistan, Kabul
AFG
Hakuna idadi ya wanajeshi wa Kimarekani wanaoweza kuusaidia mji mkuu wa Afghanistan, Kabul dhidi ya matukio ya Kiagaidi nchini humo. Na huu ndio mji wa hatari zaidi duniani. Matukio ya mabomu, kulipuliwa kwenye mahoteli na Ubalozini ni kitu cha kawaida.
2. Somalia, Mogadishu
somalia MOGADISHU
Mpaka hivi karibuni, Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ulikuwa moja kati ya miji hatari zaidi duniani. Umoja wa Mataifa walijiondoa kwenye ulinzi na usalama wa nchi hiyo baada ya Serikali tawala kuanguka mwaka 1991. Matukio ya Al Qaeda yalivuma mpaka mwaka jana ambapo wapiganaji wa Umoja wa Afrika waliingilia kati.
3. Iraq Baghdad
iraq
Iraq, Baghdad ni miongoni mwa miji ambayo sio salama pia na kwenye matukio mbalimbali ya Kigaidi hutokosa kulisikia jina lake. Lakini baada ya Marekani kuingilia kati matukio mengi yanayotokea mjini Baghdad hali kidogo imetulia. Miaka mingi ya matukio mbalimbali imeharibu miundo mbinu ya mji huo.
4. Ciudad Juarez,Mexico.
mexico
Mexico ni nchi inayofahamika kama bandari ya madawa ya kulevya duniani kupitia mji wa Ciudad Juarez. Wafanyabiashara wa madawa ya kulevya Mexico wanaogopwa na mapolisi wengi ni vijakazi wao wakubwa. Ciudad Juarez ni moja kati ya miji hatari zaidi duniani ukitoa maeneo yake ya vita.
5. Abidjan, Ivory Coast.
ivory coast
Abidjan ni mji uliopo Ivory Coast ambao kwa muda mrefu kulikuwa na matukio ya kialifu mengi sana yaliyoteka headlines mbalimbali duniani lakini baada ya kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo alievua majukumu yake kumpatia Rais aliyechaguliwa Alassane Outtara, Abidjan kidogo imetulia lakini bado unahesabika kama mji hatari.
6. Caracas, Venezuela.
venezuela1
Caracas mji mkuu wa Venezuela nao pia upo kwenye list ya miji hatari zaidi duniani na unahesabika pia kama bandari ya madawa ya kulevya. Makosa kama uwizi, kuporwa na makosa mengine madogo ni vitu vya kawaida sana kwao mapolisi hawana sauti wala nguvu ya kudhibiti vitendo hivi.
7. Sana’a, Yemen.
yemen
Mji mkuu wa Yemen, Sana’a umekuwa ukiingia kwenye headlines mbalimbali duniani kufuatia vita dhidi ya aliyekuwa Rais wa nchi Ali Abdullah Saleh. Mgogoro huo umefuatia na matukio kadhaa ya Kigaidi nchini humo na kuwekwa kwenye orodha ya miji hatari zaidi duniani.
8. Peshawar, Pakistan.
pakistan
Pehsawar mji uliopo Pakistan ni miongoni mwa miji hatari duniani, mji huu sio salama kabisa kwa wageni matukio ya kutekwa na kulipuliwa na mabomu ni matukio ya kawaida sana kwao.
9. Nairobi, Kenya.
nairobi1
Matukio ya Al Shabaab nchini Kenya pamoja na matukio mengine ya kiualifu iliiweka Kenya kwenye headlines mbalimbali. Kutembea au kusafiri usiku nchini Kenya sio salama kabisa kwani kuibiwa na kuporwa ni matukio ya kawaida.
10. Cape Town, South Africa.
cape-town
Cape Town mji uliopo South Africa ni maarufu sana kwa maeneo ya kitalii duniani, lakini ikifika usiku mji huu sio salama kabisa kwa matembezi haswa kwa wanawake. Matukio mengi ya uhalifu ni kutokana na ubaguzi wa matabaka kati ya matajiri na maskini.

0 comments:

-