Diamond na mpenzi wake Zari katika Exclusive One on One Interview ya Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds TV.
STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'
amefunguka kuwa tayari amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Zarinah
Hassan 'Zari' na anatarajia kupata mtoto wa kike mwaka huu.Diamond ameyaongea hayo hivi punde katika Exclusive One on One Interview ya Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds TV kuelekea katika shoo ya Zari All White Party itakayofanyika leo usiku katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.
Katika mahojiano hayo ambayo Diamond ameambatana na mpenzi wake huyo, ameongeza kuwa anatarajia kuingia katika ndoa mwaka huu.
Kwa upande wa Zari yeye amefunguka kuwa bado hajajua jina watakalompa mtoto wao wa kike anayetarajiwa kuzaliwa mwaka huu ila watampatia jina zuri la Kiislam na lenye mvuto.
0 comments:
Post a Comment