Philip Paul mfanyabiashara wa mishikaki ya chura katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria
Kwa wapenzi wa kula nyama choma na hususan mishikaki katika vituo vya
mabasi, mnatakiwa kuwa makini na nyama choma hiyo kwani waweza kula
mishikaki ya paka, mbwa, nyoka na sasa mishikaki ya nyama ya chura.
Mishikaki ya nyama ya chura Philip Paul ni muuzaji wa nyama
choma za chura - na yeye pamoja na mke wake na mtoto wao wa kike
wanapenda kula mishikaki ya chura. Familia hiyo inatoka jimbo la
katikati ya Nigeria la Benue lakini wanaishi kaskazini mashariki mwa
Nigeria, ambako watu hawapendelei nyama hii ya chura. Philip
mwenye umri wa miaka 25 anasema ni rahisi kuwakamata vyura kwa mikono
mitupu. Usiku anawatega kwa kuwawekea popo na vyura wanaporuka huwaendea
na kuwakamata. Baadaye anawatunga katika mti. Tangu mwaka 2008
amekuwa akifanya biashara kwa kuwakamata vyura katika jimbo la Adamawa
na kuwasafirisha kwenda jimbo la Benue, ambako mishikaki ya chura
inapendwa.
0 comments:
Post a Comment