1.DEMU WAKO WA ZAMANI.
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano
yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi,
kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya
iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna
vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo,
ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si
rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo
yatakuwa ni ya damuni. 2. DADA WA RAFIKI YAKO KIPENZI
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu
kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo
hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta
siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake.
Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo
mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa,
sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako. 3. WANAWAKE WENYE MAMBO MENGI
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha
kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote
kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu
ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote. 4. WANAWAKE WANAOPENDA ELA KUPITILIZA.
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe
kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa
zaidi. 5.DEMU WA ZAMANI WA RAFIKI YAKO Kama unathamini
urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa
demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya
yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine
inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba
ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani. Jamani wadau huu ni ushauri tu kwani mademu wapo wengi sana so unaweza kuwa na mwingine tofauti na hawa. Please SHARE NA WASHKAJ WAJIFUNZE HII |
0 comments:
Post a Comment