Monday, April 6

Need-Work 
Tatizo la ajira ni kilio cha vijana wengi TZ, watu wanalalamika kwamba wamesoma lakini hawajaajiriwa.. unadhani hili liko BONGO pekeake?
Jamaa mmoja Uingereza, Huw Davies ana degree ambayo ameipata mwaka 2002 baada ya kusoma Chuo cha Glamorgan, lakini toka amemaliza mpaka leo hii amekuwa anatafuta kazi.. ni kwamba hajaajiriwa mpaka leo.

JS60477554JPG (1)
Huw Davies
Jamaa huyo mwenye degree ya Geography amekuwa akitafuta kazi inayoendana na taaluma yake  ya masuala ya mazingira kwa miaka 13, ambapo mpaka sasa ameshaomba kazi mara 500, lakini hajawahi kuitwa kwenye Interview hata mara moja.
mer-grants
Mtaa anaoishi Huw Davies
Davies hajataka kufanya kazi nje ya Uingereza, bado ana imani kwamba atapata kazi tu siku yoyote.. kwa sasa anasema yuko tayari kufanya kazi yoyote hata ya kuendesha taxi.

0 comments:

-