Saturday, April 18


NI Jumamosi nyingine mpenzi msomaji wa safu hii ya Show The Love tunakutana kwa ajili ya kupeana darasa la uhusiano.Uzuri wa mapenzi ni kuridhishana. Kila mmoja ‘ainjoi’ kukutana na mwenzake, alifurahie tendo katika hali ambayo hawezi kuwa na hamu ya mapenzi pindi mnapokuwa mmemaliza tendo.
Kinyume na hapo, kukiwa na tatizo katika upande mmoja, furaha ya tendo inaondoka. Mmoja kati ya wapendanao anakuwa na shauku ya tendo wakati mwingine hana. Kitakachofuata hapo ni yule ambaye hajaridhika kutafuta njia mbadala ili kupata tiba ya mapenzi.
Mwanaume anaweza kuwa anataka kumridhisha mpenzi wake lakini anashindwa au mwanamke anataka kumridhisha mpenzi wake lakini inashindikana.Wanapokutana faragha, kila mmoja anakuwa na nia njema kabisa kutaka kukamilisha tendo la ndoa lakini tatizo linakuwa kwa mmoja wao na kuwafanya washindwe kufurahia tendo.

Mmoja kati ya wapendanao anakuwa anawahi kuridhika wakati mwenzake anakuwa bado hajafikia muda wa kuridhika.Hapa ndipo zinapoibuka zile kauli za ‘mwenzangu haniridhishi’, ‘mwenzangu amekuwa gogo’ na nyingine nyingi zinazofanana na hizo.
Yule ambaye haridhishwi huwa anakuwa katika wakati mgumu. Kutokana na desturi ya watu kutopenda kuambiana ukweli hususan katika jambo hili ambalo wengi wanaamini ni la aibu, hubaki nalo jambo hilo moyoni na kuendelea kuumia.
Anavumilia hadi inafika wakati anachoka. Kinachofuata hapo ni kusaka suluhu. Ndiyo wakati wa kuanza kuwatafuta marafiki tofautitofauti ambao wanaweza kumshauri vizuri au vibaya.Wapo wanaoweza kumshauri kwamba afanye vitu fulanifulani ili aweze kufanikiwa lakini wengine huweza kumshauri atafute mtu mwingine ambaye atamridhisha. Kutokana na kero anayoipata, ni rahisi tu kufanya maamuzi ya kujaribisha kwa mtu mwingine.
Usaliti ndiyo unaanzia hapo. Amani inatoweka na baadaye ugomvi huibuka, hapo ndipo watu hufikia hatua ya kushindwa kuvumiliana na hatimaye kuachana.Kinachotakiwa kufanyika endapo suala kama hili linapotokea kwanza ni kuzungumza na mwenzako. Kama unaona kuna kitu hakipo sawa kwa upande wako, mueleze mwenzako ili muweze kutafuta suluhu.
Kama pia tatizo unaliona lipo kwa mwenzako, tumia lugha nzuri kumueleza ili muweze kupata suluhisho.
Yawezekana tatizo ambalo upo au yuko nalo ni la kimahesabu tu ya tendo. Tendo hili linapaswa kufanyika kimahesabu ili muweze kwenda sawa.Yawezekana mwenzako anakurupuka, kabla hajakuandaa yeye anakuwa tayari ameshafika mbali kifikra hivyo kujikuta anakuacha kwenye mataa.

Jadilini kwa kuelezana nini kifanyike ili kila mmoja afahamu. Ushirikiano wa kulifanya tendo liwe na mashamsham unatakiwa.Ujue wapi mwenzako anapenda umguse zaidi na kwa namna gani. Ni vyema mkawekana wazi ili kila mmoja asiwe mgeni na mwenzake.
Ukimya wakati mwingine ndiyo unasababisha matatizo ya wapendanao kutofautiana. Yawezekana ulilonalo au alilonalo mwenzako ni la kitabibu, waweza kwenda kutibiwa hospitali na likaisha. Mueleze mwenzako, mtashauriana na kupata suluhu. Hakuna haja ya kuhangaika kwa kutafuta suluhu ya kuridhishwa na mtu mwingine. Unaweza kufanya hivyo kumbe nako bado likawa tatizo ni lilelile.
Utahamia kwa mwingine bila kujua kiini cha tatizo huenda ni wewe mwenyewe, matokeo yake yatakuwa ni yaleyale.Au pengine tatizo ulilonalo au alilonalo mpenzi wako linahitaji tiba ya kidaktari, ni vyema ukazungumza na mwenzako na kufunguana mawazo.Kwa leo tuishie hapo, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri!

0 comments:

-