Wednesday, April 1

rip-786x305 
Mzee mmoja amepigwa huko Kimara Dar, baada ya kijana aliyekuwa anaishi nae ambae ni mtoto wa kaka yake aliyekuwa dereva bodaboda ambae alipata ajali na kufariki, wakati wa mazishi mzee huyo akakataa maiti isipelekwe nyumbani kwake kwa madai kuwa anamdai marehemu.
Kijana ambae ni rafiki wa marehemu amesema Mzee huyo alikataa maiti isiingie nyumbani kwake kwa madai kuwa ni uchuro na anamdai marehemu shilingi laki tatu, wakavunja geti na kuingia ndani lakini bado aliwakatalia ndipo walipoamua kwenda uwanja wa mpira kwa ajili ya watu kupata nafasi ya kuaga.

Baadae alikuja Mwenyekiti akamshauri aende uwanjani kuaga alipofika vijana hao walianza kumpiga na kumzuia kusafiri na mwili wa marehemu, kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi.
Mzee huyo alipofatwa ili kujua sababu ya kukataa maiti isiingie ndani kwake alikataa kuzungumza.

0 comments:

-