Kutokana na shambulio la kigaidi katika chuo cha Garissa kilichopo Kenya,
baadhi ya familia bado hawajui watoto wao waliko, mzazi mmoja amesema
aliongea na mtoto wake hadi dakika ya mwisho akiwa mikononi mwa magaidi
hao baada ya kukamatwa.
“Alikuwa
akininong’oneza akiniambia
yuko chini ya kitanda akaniambia tuu
tumuombee akakata simu, saa sita na nusu nikaona hiyo namba ikinipigia
nilikuwa naongea naye akaniambia nimeshikwa sina la kufanya akaniambia
ndio hawa hapa silaha zao tunaziona, sijui ni bunduki sijui ni silaha
gani walikuwa nazo
Akaniambia
ndio wanataka kuongea na baba lakini baba amepatikana wako busy sana
wanamharasi, tukaongea nae kidogo wakamnyang’anya simu nikaongea na hao
magaidi Al Shabaab …
Akiendelea kusimulia; “wakaniambia
wee mzee nakupa dakika mbili apige Somalia, akaniambia wee mzee
umeshindwa kupiga simu? Kama umeshindwa kupiga simu acha mwanao asali
maombi yake ya mwisho mi nasikiliza tu.. akasali maombi yake yote
akaniambia umesikia amemaliza kuomba what next we sikiliza, sikiliza
mwenyewe hesabu mwenyewe risasi naua kabisa nikasikia three gunshot… na
akaniambia nimeuwa chimbeni shimo”– aliongea mzazi wa mwanafunzi mmoja aliyeuawa.
Tukio hili limesababisha wanafunzi 147 kufariki na wengine kujeruhiwa, kwa sasa Chuo hicho cha Garissa kimefungwa kwa muda.Pole kwa wote ambao wameathirika kutokana na tukio hili, #RIP watu wetu waliofariki.
0 comments:
Post a Comment