Kuna
tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa, lakini leo nimekuja na hii list
ya Marais nane wanaoongoza kwa kuwa na utajiri mkubwa zaidi ya wenzao
Afrika.
Ukiachilia mbali marais wengi wa Afrika
kupenda kukaa kwa muda mrefu madarakani lakini kuna hili la
kujilimbikizia mali, wengine huzipata kabla ya kuwa marais lakini wengi
wao huzipata wakati wanashikilia madaraka kwa kipindi chote wanapotawala
nchi husika.
Jose Eduardo Dos Santos ndiye Rais anayeongoza kwa utajiri Afrika kutoka Angola, aliingia madarakani mwaka 1979, ana utajiri wa dola bilioni 20
Mohammed V1 Ni Mfalme wa Morocco ambaye amekaa madarakani kwa miaka 15 ,, ana utajiri wa dola bilioni 2.
Teodoro Obiang Nguema Mbasogo: Rais
huyu wa Equatorial Guinea aliingia madarakani 1979, ana una utajiri wa
dola milioni 600 licha ya wananchi wa nchi hiyo kuishi maisha ya
kimaskini kutokana na uchumi wao kuwa chini
Uhuru Kenyatta ni
Rais wa Kenya ambaye alichaguliwa mwaka 2011, ana utajiri wa dola
milioni 500, mbali ya kuongoza nchi ana vyanzo mbalimbali vya utajiri
ikiwa kuwa na hisa nyingi katika kampuni mbalimbali,benki na mahoteli
makubwa ya kifahari.
Paul Biya ni
Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982, ana utajiri wa dola milioni 200,
unaambiwa ndiye rais anayetumia kiasi kikubwa cha pesa katika ziara zake
kuliko marais wote duniani na hutumia euro 30,000 kwa siku katika ziara
zake
King Mswat iii Ni
mfalwe wa Swazland akiwa na utajiri wa dola milioni 100, anashika
nafasi ya 15 katika familia za kifalme tajiri duniani, Unaambiwa wake
zake 13 hutumia zaidi ya dola milioni sita kufanya manunuzi yao pekee,
pia Serikali yake hutenga bajeti ya dola milioni 61 kila mwaka kwa ajili
ya matumizi ya nyumbani
Idriss Derby Ni Raisi wa Chad tangu mwaka 1990 na ana utajiri zaidi ya dola milioni 50
Robert Mugabe wa Zimbabwe, ana zaidi ya miaka 26 akitawala nchi ya Zimbabwe, utajiri wake ni dola milioni 10
0 comments:
Post a Comment