Hiki ndicho alichopanga kukifanya mwimbaji wa
muziki wa dansi ambaye mara nyingi hupenda kusimama kama ‘solo artist’,
Christian Bella kwa ajili ya kukuza soko la muziki wa dansi Tanzania,
akifuata nyayo za wasanii wa Bongo Fleva.
Bella amesema kuwa kuanzia Februari mwaka huu,
atatengeneza video kubwa itakayoongozwa na mtayarishaji God Father
nchini Afrika Kusini.
“Kwa nafasi niliyonayo sasa, nikiendelea na video
za ‘kitoto’ nitafeli, natoa wimbo mmoja matata nitakaoanza nao mwaka,
mwanzoni mwa Februari utakuwa tayari.
Namwomba Mungu mipango yangu iende kama
nilivyopanga, ikiwamo kufanya video kubwajapokuwa zina gharama kubwa na
mimi sitaangalia suala hilo, nataka mafanikio, hivyo lazima nijilipue
ili kujitangaza kimataifa,” alisema Bella.
Bella alisema kwa sasa ameshatenga kiasi kikubwa
cha fedha ili akamilishe mpango huo, kwani anaamini akitayarisha video
kubwa, itakuwa rahisi kazi zake kuonyeshwa katika televisheni kubwa
Afrika kama MTV Base, Channel O, Trace na kwingineko.
“Najua gharama yake inaweza kufika kiasi cha Sh68
milioni. God Father ndiye mtayarishaji nayemlenga kwa sasa, gharama hiyo
ni video tu pasipo kuangalia mambo mengine, ikiwamo usafiri, mavazi na
vitu vingine muhimu,” alisema.
Alisema uamuzi huo umetokana uchunguzi alioufanya pamoja na ushauri kutoka kwa watu kadhaa, wakiwamo wadau wa muziki.
“Mwaka huu sifanyi kawaida kama miaka iliyopita,
kwa sababu tunakoelekea lazima tuangalie mwelekeo wa dunia, nini
kinahitajika ili kufikia malengo ya kufanya vizuri.
“Ndoto yangu ni kutengeneza pesa, lakini hilo linawezekana kama nitafanya jitihada,” alisema Bella na kuongeza:
“Kwa mfano, leo wamemtambua Diamond Platnumz katika Channel O, Trace, BET kwa sababu ya video kubwa.
Haimaanishi kwamba Diamond anafanya muziki mzuri
kuliko wasanii wote Tanzania hapana, lakini tunampongeza na kumuunga
mkono na kumpa hongera kwa kuthubutu vitu vikubwa kama hivi, mtu
anayeanza na anayefanya vizuri lazima umpongeze na wewe upite palepale.”
Alipoulizwa kuhusu umahiri wake katika tungo mbalimbali za
mashairi na sauti yake yenye kuvuta hisia za mashabiki wa muziki wa
dansi, Christian Bella alisema huchukua miezi kadhaa kutunga mashairi ya
wimbo mmoja.
“Sikurupuki, inachukua muda mrefu, linaweza kuja
wazo la mrindimo kwanza likakaa kichwani, baadaye nikarekodi kidogo
kwenye simu nauacha naanza kutafuta meneno kidogo kidogo siyo kwa
haraka.”
Alisema kuna nyimbo zingine za haraka ambazo,
huingia studio siku hiyohiyo akatengeneza wimbo mara nyingi huwa
‘kolabo’ na siyo nyimbo zake.
“Nyimbo zangu zinachukua muda, natulia na wazo, nafikiria nini cha kufanya, sina haraka kufikia kutoa uamuzi,” anasema.
“Wakati mwingine nakaa na mtu na kuanza kumuuliza
hivi hapa nifanye nini ili wimbo uwe bora nikiimba...Hivi naeleweka,
nachunguza na kufanya utafiti kabla ya kuwalisha mashabiki.”
Ingawa hutumia miezi kukamilisha wimbo mmoja,
Bella alisema anaweza kuimba mwanzo hadi mwisho katika mtindo wa moja
kwa moja ‘freestyle’.
“Naweza kuimba ‘freestyle’, lakini linapokuja
suala la kurekodi, lazima niifikirie kwanza inapendeza, inafaa kwa
jamii, mfano wimbo Nakuhitaji niliouanza kama Rhumba, lakini kuandaa
mdundo unaitwa mutwashi ndiyo
0 comments:
Post a Comment