Sunday, December 14

wedding-cake-lovely-minimalist-modern-two-tier-black-and-white-wedding-cake-with-gorgeous-red-roses-topper-extraordinary-modern-wedding-cakes-collection
Sherehe moja kubwa ya harusi iliyopangwa kufanyika Turkana, Kenya iliingia majonzi makubwa saa chache kabla ya sherehe hiyo kufanyika.
Binadamu tumekuwa tunapanga mengi kwenye maisha wakati Mungu anapanga yake pia, yale yote yaliyopangwa kufanyika siku ya Harusi hiyo ikiwemo kukata keki pamoja na burudani ya waimbaji wa kwaya, ililazimika yafanyike siku ya msiba wa Peter Eroo
ambaye ilikuwa awe Bwana Harusi kwenye ndoa hiyo huku ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye simanzi kubwa.
Bibi harusi Perpetua Abenyo  alikuwa kwenye wakati mgumu lakini hakuwa na jinsi ya kupingana na ukweli kwamba mtu aliyekuwa awe mume wake hakuwa naye tena, mauti yalimkuta Jumamosi iliyopita baada ya kuugua ghafla na kufariki saa chache kabla ya ndoa yao.
Mazishi ya Peter yalifanyika jana December 12, Perpetua akisema imani yake haitoyumba na anaamini kila kitu ni mipango ya Mungu.
Unaweza kuisikiliza Habari ambayo nimekurekodia kutoka Citize Tv pamoja na kuangalia video ya taarifa hiyo na kuitazama. Unaweza kuisikiliza.



0 comments:

-