Mwanaume
mwenye umri wa miaka 33, raia wa Ufaransa amefungwa jela kwa kosa la
kumsumbua mpenzi wake wa zamani kwa kumpigia simu mara 21,807 akimtaka
amshukuru kwa kukarabati nyumba waliokuwa wakiishi.
Mwanaume
huyo alikiri kufanya kosa hilo na kueleza kuwa ulikuwa ‘upumbavu’ kwa
kuwa alikuwa amekatazwa kuwasiliana na mpenzi wake huyo wa zamani kwa
kipindi cha miezi kumi iliyopita na akakubali.
Pamoja na kifungo hicho, ameamriwa kuhudhuria matibabu maalum ya akili na marufuku ya kuwasiliana tena na mwanamke huyo.
Mwanaume
huyo aliwahi kulazwa hospitalini kutokana na msongo wa mawazo wakati
akijaribu kuendana na hali halisi baada ya kuachwa na mpenzi wake huyo
mwaka 2011.
“Muda
ule, mantiki yangu ilkuwa hadi arudishe pesa nilizotumia kukarabati
nyumba yetu…au angalau aseme ‘asante’, nisingeweza kuacha kumpigia
simu.” Aliiambia mahakama ya Lyon.
Imedaiwa
kuwa kwa siku moja mwanaume huyo alikuw akipiga simu na kutuma messages
zaidi ya mara 73 kwa siku hali iliyogeuka kuwa usumbufu mkubwa.
0 comments:
Post a Comment