Wednesday, September 3

 
Baada ya watu kadhaa kulipotiwa kuwa wamefariki nchi jilani ya Congo kwa ugonjwa wa ebola wananchi Mkoani Iringa wametakiwa kuchukua tahadhari ya maambukizi na athari za ugonjwa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma amesema Mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa ya kusini mwa Tanzania ambayo inapakana na nchi za nje pia inapitiwa na barabara kuu inayotumika na wafanyabiashara wa kigeni wakiwemo wa kutoka nchini Congo.
Kwa upande wa Daktari wa Mkoa wa Iringa Bw. Robert Sami amesema ugonjwa huu huenezwa kutokana na kugusa damu, viungo na majimaji ya mtu au baadhi ya wanyamapori kama nyani, nungunungu na popo ambao wamegundulika kuwa na virusi vya ugonjwa huo.
Bw. Sami ameongeza kuwa dalili za ugonjwa huo ni homa ya ghafla, kuishiwa nguvu,maumivuya misuli, kuumwa kichwa, kuumwa koo, kutapika, kuhara ambapo mwishowe hupelekea figo kushindwa kufanya kazi pamoja na kutokwa na damu ndani na sehemu za wazi za mwili wa binadamu.
Aidha amesema hospitari ya Mkoa wa Iringa imepokea msaada wa vifaa kutoka wizara ya afya kitaifa kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa pia wameanzisha mafunzo kwa wauguzi juu ya matibabu na kujikinga na ugonjwa huo.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa Dkt. Ishengoma amesema kutokana na kuongezeka kwa vifo vya ugonjwa huo kwa nchi za Afrika ya kati hivyo amewataka wakazi wa Mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla kufuata ushauri wa wataaramu wa afya juu ya kuepukana na ugonjwa hu


0 comments:

-