Kamanda Justus Kamugisha
Mtoto
aitwaye Happiness Kashindye mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa
darasa la tatu katika shule ya msingi Negezi iliyopo kata ya Ndala
Manispaa ya Shinyanga ameuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa
macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani.
Tukio
hilo la kusikitisha limetokea jana saa saba mchana katika kitongoji cha
Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi ambapo mwili wa marehemu
ulikutwa kichakani.
Kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja
amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo alibakwa na kutobolewa macho.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa huku akitoa
wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini na kuwakamata
wauaji ili hatua za kisheria zichukuliwe.
0 comments:
Post a Comment