Katika
mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri
wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza
azma hii waombaji watajaza kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya
vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya Polisi kwa njia ya Posta kabla ya
tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo:
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM
Waombaji wawe na taaluma zifuatazo:
Shahada: Menejimenti
ya Rasilimali Watu, Utawala katika Utumishi wa Umma, Uchumi, Saikolojia
na Ushauri Nasihi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji[BaLE], Sheria,
Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa Habari, Uandishi wa Habari za
Michezo, Mawasiliano ya Umma, TV & Redio Production, Michezo,
Ugavi[BA in Procurement & Supplies], Mawasiliano ya Redio[Bsc in
Radio Communication], Mazingira[BA in Environmental Disaster Mgt],
Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining Engineering], Uchoraji[BA in
Fine Arts], Fedha na Benki[Finance & Banking], Daktari[Medical
Doctor] na Daktari wa Meno[Dental Surgeon], Mkemia, Bailojia[Molecular
Biology].
Stashahada: Utunzaji
Kumbukumbu, Katibu Muhutasi[Personal Secretaries], Mawasiliano ya
Redio, Matengenezo ya Kompyuta, Fax na Photocopy Machines, Mafundi
Mitambo wa Meli, Mafundi Umeme wa Magari, Ugavi[Procurement &
Supplies], TV na Video Production, Manahodha, Tabibu[Clinical Officer],
Tabibu wa Meno[Dental Therapist], Mzoeza
Viungo[Psysiotherapist/Occupational Therapist], Fundi Sanifu
Mionzi[Radiographer] na Fundi Sanifu Macho[Optometrist].
Astashahada: Uzamiaji, Mpishi, Fundi Pikipiki, Fundi Ushonaji na Muuguzi Msaidizi[Enrolled Nurse]BOFYA HAPA KU APPLY>>
0 comments:
Post a Comment