Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani
Na James Festo, Njombe.
KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani pamoja na
dereva wake Nuaka Seme wamelazwa katika hispitari ya Mkoa wa Njombe ya
kibena ambako wanaendelea kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea
usiku wa kuamkia jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo
katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia
papo hapo.
Akiongea na vyombo vya habari huku akipatiwa matibabu katika hospitari
ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP
Yahaya rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda
Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa
nne za usiku katika barabara ya Makambako hadi Njombe.
Aidha Jeshi la Polisi limesema kuwa katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George Stephano Matiko (24)
H580 Pc George Enzi za uhai wake.
Nuaka Sema aliyekuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili PT 2058
alisema kuwa kutokana gari hilo la mizigo kukaa katikati ya barabara
walishindwa kupishana kwa wakati na kuligonga kwa nyuma na baadae
kukutana uso kwa uso na nguzo ya umeme iliyowasababishia ajali.
"ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full
light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria
hatari na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande
wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda
tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.
Aliongeza kuwa " mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga
nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana
wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na
lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".
Kwa upande wake Afisa muuguzi wa hospitari hiyo Bw. Denis Haule
alisema kuwa majeruhi wawili walipokelewa majira ya saa tano usiku na
mwingine alikuwa amekwisha fariki dunia na kubainisha kuwa hali ya
majeruhi hao inaendelea vizuri na Kamanda wa Polisi anaweza kuruhusiwa
muda wowote.
"tumewapokea jana usiku majeruhi wawili na mmoja akiwa amekwisha
fariki dunia , hali yao kwa sasa inaendelea vizuri na kamanda anaweza
kuruhusiwa wakati wowote....lakini dereva wake anatakiwa kuendelea
kupewa matibabu kutokana na maumivu mbalimbali katika mwili wake
0 comments:
Post a Comment