Wakati wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wa kususia vikao vinavyotarajiwa
kuanza leo mjini Dodoma, mmoja wa wajumbe wake jana aliripoti bungeni
na kujiandikisha.
Mjumbe huyo, Clara Mwatuka ambaye pia ni Mbunge wa
Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa 6:30 mchana
akiwa ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde
(Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).
CUF ni moja ya vyama vinavyounda Ukawa, pamoja na
Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo, Profesa
Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wametangaza kwamba
wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki vikao vya Bunge
hilo.
Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Bwanausi.
Awali, alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu
kuwapo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha
bungeni.
0 comments:
Post a Comment