Saturday, August 30



WAKATI NAINGIA FACEBOOK KITU CHA KWANZA KABISA KUKUTANA NACHO NI HII MAKALA KUHUSU BETTY,,BAADA YA KUISOMA NIKASEMA MAYBE NOW WATU WATAELEWA MADHARA YA CYBERBULLYING NA INASKITISHA KUWA KIFO CHA MTU NDO KIWE MFANO KWANINI LAKINI,,

YAANI HILI NDIO TAIFA LA KUJIVUNIA KUWA HIVI NDIVYO TUMEKUWA KWELI??JE HUYU ANGEKUWA MTOTO WAKO,AU NDUGU SASA HIVI UNAJISKIAJE WAKATI NA WEWE PIA NI FOLLOWER WA MAPAGE KIBAO HUKO INSTANGRAM,,AMKENI NA MBADILIKE HUYU NI MTOTO SANA KUPOTEZA MAISHA YAKE KIUKATILI HIVI,REST IN PEACE BETTY NDEJEMBI!!

kapumzike kwa amani na uwasemehe walioshindwa kukuface na kukwambia kama umewaudhi bali wakachukua hatua nyengine na kufanya ukatili

jamani msifikiri kila mtu yuko strong binadamu tunatofautiana istoshe huyu dada akuwa na wazazi na sometimes wazazi wetu plays a big part kwenye maisha yetu,,yaani kaniuma huyu mtoto utadhani namjua but haina haja kiubinadamu WE FAILED YOU BETTY,,




Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakubadilishi ukweli kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.

Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi watu wamesema mengi, na yameandikwa mengi. Kila mmoja kwa namna alivyoguswa. Zitto Kabwe ametweet hivi asubuhi "Justice for Betty", akitoa rai haki ipatikane kwenye kifo cha Betty.
Jokate Mwegelo nae ametweet kuomba msaada wa kuchunguza kifo cha Betty. Na watu wengine maarufu kila mmoja kasema neno, labda kwa sababu Betty alikua maarufu in one way or another.
Lakini hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake, alinyanyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo chake, lakini mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.
Saa chache kabla ya kifo chake Betty alitweet kua "PINDA HAWEZI KUWA RAIS". Baada ya kutweet hakuonekana tena hadi alipookotwa mtaroni kesho yake asubuhi akiwa amefanyia vitendo vya kikatili na akiwa amepoteza fahamu.
Lakini kabla hata ya kutweet hivyo, Betty alikua anaandamwa sana mtandaoni huko Twitter. Kuna watu walianzisha team ya kumtukana, kumjibu hovyo na kumprovoke kwa kila alilofanya.
Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu kwa Betty kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususani cha mtu maarufu.
Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki. Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa kujifanya askari JKT, kusengenya na kupost majungu.... Aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza.
Kwenye hii mitandao, matusi imekuwa njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, Facebook na Instagram lakini ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'
Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo.
Marehemu Betty ni victim wa yote hayo. Alitukanwa sana, na aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria, superstar uchwara etc.. and i hope hao waliomuita hivyo wanajifahamu na wengine wananisoma hapa.
Japo sijui chanzo cha 'ugomvi' wao, lakini naamini kuna watu wengi tu waliokuwa 
katika nafasi ya kuzima moto huo kwa vile walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika lakini kwa sababu ya unafiki wakapalilia moto maana wanafurahi watu wakigombana.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni UNAFIKI. Watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. 
Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa kwamba 'wakati muafaka wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.'
Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali.
Mojawapo ya Tweet za mwishomwisho za marehemu alisema hivi "Do I have a sister to support me? No. Do I have a Dad/Mom to run to or support me. No. Im hurting and wanna cry? Yes. BUT I know God is watching"
Haihitaji degree ya Saikolojia kujua kuwa Betty alikua kwenye kipindi kigumu mno na alihitaji msaada kwa watu waliokua karibu yake. 
Betty anauliza"Nina dada wa kunisaidia? Hapana. Nina baba au mama wa kumkimbilia? Hapana. Nimeumizwa/nina uchungu na ninahitaji kulia (lakini nitamlilia nani?). Ila najua Mungu anaona"
Kwa bahati mbaya Betty hakuwa na baba, hakuwa na mama, hakuwa na dada wala kaka. Wote walishatangulia mbele ya haki. Alibaki peke yake, peke yake na Mungu wake.
Lakini binadamu wasivyo na aibu wala huruma wakazidi kumtukana na kumsimanga, huku wengine wakiporomosha matusi mazito. Hawakujua yaliyokua moyoni mwake. Wakamtambia kwa maisha mazuri wanayoishi na namna walivyobarikiwa.
Betty akiwa katika maumivu makali ya hisia akapost hivi "Thank you all for the names i was called, luck y'all have such a perfect life.! No hard feelings.. Im alive still.! Endeleeni kuongea"
Kwa tafsiri isiyo rasmi Betty alisema "Asanteni kwa majina yote mliyoniita. Mmebarikiwa kuwa na maisha mazuri.! Hamuumizwi na hisia kama mimi. Ila bado ninaishi, endeleeni kuongea"
Kwa bahati mbaya hakuna aliyejali, hadi juzi asubuhi (jumatano) Betty alipookotwa kwenye mtaro akiwa amefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na akiwa amepoteza fahamu.
Kifo cha Betty ni miongoni mwa vifo vya kikatili sana kuwahi kutokea nchini. Nashauri wanaharakati ea haki za wanawake wapambane kuhakikisha haki inapatikana. Akina Annanilea Nkya, Hellen Kijobisimba watafute haki ya binti huyu kzma Zitto Kabwe alivyosema "Justice for Betty"
Imagine mtu aliyekua kwenye maumivu makali ya hisia, anatekwa na genge la wahuni. Bila kujali kipindi kigumu alichokua anapitia, bila kujali hakua na wazazi, bila kujali psychological toacher aliyokua nayo still wanamfanyia unyanyasaji wa kijinsia hadi anapoteza fahamu.
Betty aliokotwa mtaroni na kupelekwa hospitali. Jana (alhamisi) aliweza kufungua macho, lakini hakuweza kuongea lolote hadi saa 3 usiku wa kuamkia leo, mauti ilipomkuta.
Kwaheri Betty, kwaheri classmate wangu (Majengo sec), kwaheri rafiki, kwaheri ndugu. Umeondoka dunia bado inakuhitaji. Naumia u have gone too young, lakini naumia zaidi coz umekufa kikatili mmno. Japo sijui nitakufaje, lakini nadiriki kusema hukustahili kifo cha aina hii.
Nakumbuka sms yako ya mwisho kwangu uliniambia hivi " blv me, only youths can change this country". nilipopata taarifa ya kifo chako nimerudia kuisoma sms yako mara mbilimbili. Sikujua kua sms hiyo ndo ulikua unaniaga. 
Umeniaga kwa kutuachia vijana wosia, kuwa vijana pekee ndio wenye uwezo wa kuibadilisha nchi hii. Nitakua nimekusaliti ikiwa sitautendea kazi wosia huu. I promise to fight and motivate other youths to liberate this country for ur dedication.
Umekwenda kumfuata mama yako, umemfuata baba yako. Wazazi wako walitangulia, leo wewe umewafuata. Hatimaye familia nzima mmekutana Paradiso.. Pumzika kwa amani Betty.!

0 comments:

-