Mwandishi Wa Makala Happiness Katabazi
-------
KATABAZI : NIMEACHA KAZI GAZETI LA TANZANIA DAIMA
KATABAZI : NIMEACHA KAZI GAZETI LA TANZANIA DAIMA
: KWASASA NI OFISA HABARI CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO(UB)
MIMI
Happiness Thadeo Katabazi (35), Leo Agosti 29 mwaka 2014 ndiyo siku
yangu ya mwisho ya kufanyakazi Katika Gazeti la Tanzania Daima.
Nimeachakazi
kwa Hiari yangu katika Gazeti la Tanzania linalotolewa na kampuni ya
Free Media Ltd kwasababu Agosti Mosi Mwaka huu,niliwasilisha notisi
ya kuacha Kazi na ombi hilo lilikubaliwa na waliokuwa wakubwa wangu
wa Kazi.
Kwa
heshima na taadhima napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mwenyezi
Mungu Kwani alinipa Afya,Nguvu na maarifa nikaweza kulitumikia Gazeti
la Tanzania Daima kwa Miaka nane sasa kwa uaminifu na uadilifu wa Hali
ya juu.
Kwasababu
kwa Kipindi chote nilichofanya Kazi Kama Mwandishi wa Habari wa Gazeti
Hilo sijawahi kuandika habari ambayo ilisababisha gazeti Hilo lifnguliwe
kesi mahakamani.Namshukuru Mungu Katika Hilo.
Pia
namshukuru mmiliki wa Gazeti la Tanzania kwani bila yeye kuanzisha
Gazeti Hilo nisingepata ajira na limenilea. Napenda kuwashukuru
wafanyakazi wote wa gazeti hilo kwani tuliweza kufanyakazi pamoja licha
wakati mwingine ilikuwa ikitokea Hali ya kutofautiana misimamo Katika
baadhi ya mambo mbalimbali lakini yaliyopita Si ndwele tugange yajayo.
Navishukuru
vyombo vyote vya dola ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kwani baadhi ya maofisa wa
vyombo hivyo walikuwa wakinipa ushirikiano wa kutoka Katika Kazi yangu
ya uandishi wa Habari za mahakamani kwa Miaka 16 sasa.
Nimevitaja
vyombo hivyo Vya dola Kwani Mwandishi makini na mjanja wa Habari za
mahakamani nilazima afanyekazi kwa kutegemea Polisi, Askari Magereza na
TAKUKURU.
Nawashukuru
sana Askari na maofisa wote wa majeshi hayo Kwani tukifanyakazi pamoja
na nilijifunza mambo mengi sana kutoka kwenu.Mungu awabariki na
nitaendelea kuthamini mchango wenu Kwangu Kwani mlinifundisha mengi
hasa Askari wa Jeshi la Polisi " Manjagu".
Navishukuru
vyama Vya siasa Chama Cha Malpinduzi( CCM), CUF, NCCR- Mageuzi ,
Tanzania Labour Party , DP na vingine Kwani katika Kipindi chote Cha
Kazi yangu ya uandishi wa Habari niliweza kufanya Navyo Kazi kupitia
viongozi wa juu,Kati na wanachama wa vyama hivyo.
Kwa
namna ya kipekee napenda kuishukuru Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka(DPP), iliyokuwa ikiongozwa na DPP aliyemaliza muda wake hivi
karibuni, Jaji DK.Eliezer Feleshi Kwani ni yeye Jaji Feleshi na timu
yake ya Mawakili wa serikali walikuwa wakinipa ushirikiano Katika Kazi
yangu ya uandishi wa Habari za mahakamani kwa Miaka Saba yote aliyokuwa
ameshika wadhifa huo wa DPP.Namshukuru sana Jaji Feleshi Mungu ampe
Maisha Marefu Kwani Jaji Feleshi yeye binafsi alikuwa ni Mpenzi wa
makala na Habari zangu za mahakamani na alikuwa akinikosa nilipokuwa
naandika Habari ambazo alikuwa anaona kisheria zina madhara.
Naushukuru
uongozi wa Mhimili wa Mahakama nchini chini Jaji Mkuu Mstaafu,
Agustino Ramadhani na Jaji Mkuu wa sasa Mohamed Chande Othman kwasababu
kuna baadhi ya Majaji, wasajili,makarani, walinzi wa Mahakama na
watumishi wa Kada mbalimbali wa Mahakama walinipa ushirikiano na
kunifundisha mambo mbalimbali ya jinsi mahakama na serikali inafanyaje
kazi bila kuchoka wakati nilipokuwa mwanadishi wa habari za bila kuchoka
wakati nilipokuwa naandika Habari za mahakamani.
Pia
navishukuru Vyanzo Vyangu vingine Vya Habari ambavyo ni Mawakili wa
kujitegemea,walalamikaji, washitakiwa walipo nje kwa dhamana na waliopo
magerezani walikuwa wakinipa taarifa mbalimbali kuhusu Kesi mbalimbali
na kuaniarifu mapema Kuwa siku Fulani mahabusu waliopo Katika baadhi ya
magereza watagoma lini , nawashukuru sana.
Hata
hivyo nayashukuru makundi mengine yote yaliyokuwa yakinipa ushirikiano
Katika Utendaji wangu wa Kazi. Pia na washukuru wasomaji na wapenzi wa
makala zangu na Habari za mahakamani Kwani kwa Kipindi chote hicho
mlikuwa mkisoma makala na Habari zangu wengine mlikuwa mkinipinga na
wengine mlikuwa mkiniunga mkono.
Licha
ya kuacha Kazi Gazeti la Tanzania Daima, napenda Kusema wazi Kuwa Kazi
ya uandishi wa Habari hasa uandishi wa Habari za mahakamani ' umbea'
ipo Kwenye Damu yangu, nitaendelea kuandika makala na kuchangia mijadala
tofauti kupitia mitandao ya kijamii bila kuvunja Sheria za nchi.
Kwa
sasa nimepata Kazi Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB) na Makamu Mkuu wa Chuo
hicho ni Profesa Balozi Costa Ricky Mahalu, chenye makao makao yake
makuu Mikocheni kwa Warioba, Kama Afisa Habari wa Chuo Kikuu hicho.
Nawakaribisha
waandishi wa Habari wenzangu hasa wale waandishi wa Habari za
mahakamani na wananchi wengine waje UB, ili waweze kupata elimu za
fani mbalimbali maana Ulimwengu wa sasa bila elimu ni tabu sana.
Waandishi
wa Habari tukiitikia wito wa kukubali kwenda kujiendeleza kielimu
Katika vyuo vikuu, ni wazi tutaondokana na tabia ya kukubali kutumiwa
vibaya na Makundi yanayoasimiana kisiasa, Kibiashara kuchafua watu
kupitia Karamu zetu, kujazana Ujinga ndani ya vyumba Vya Habari .
Nafahamu
neno Hilo linaweza kuwakera baadhi ya waandishi ambao hawataki
Mabadiliko na hawataki kujiendeleza kielimu kwasababu ya kijinga Kuwa
akienda shule kusoma Atakosa ' mishiko, safari'.Sijali, naamini nimesema
kweli na Mungu atanilinda na inawezekana ukiamua.Mimi ni shahidi wa
Hilo Kwani Mwaka 2009 -2010 nilipoanza kusoma kozi ya Cheti Cha Sheria
Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, kuna baadhi ya waandishi wenzangu
walinicheka na kuniona chizi lakini nikamaliza Mwaka 2012- Juni 2013
nikasoma Diploma ya Sheria Katika Chuo Kikuu Cha Bagamoyo nikamaliza
waliokuwa wananicheka Wakaanza kuniambia Kuwa walifikiri nilikuwa
natania wakati nawaaga na kwenda Kusoma Sheria.
Waliposikia
na kuniona Septemba Mwaka 2013 nimeanza kusoma Shahada ya Sheria
wameishia Kusema Kuwa Kumbe nimedhamiria, na kwamba Mimi ni mwanamke wa
Shoka na kwamba nitafika Mbali.Nawatazama kwasababu hawafahamu nawaza
nini na ni kwanini MUNgu ananipa Nguvu na uwezo wa kusoma hivyo wakati
Nasoma kwa tabu sana na kugeuka ombaomba wa Ada" Matonya'.
Licha
Nasoma shule kwa dhiki na tabu lakini siku zinakwenda na shule ndiyo
MUNgu akipenda Julai Mwaka 2016 nitamaliza Shahada ya kwanza ya
Sheria.
Nimelazimika
kujitolea mfano halisi Mimi licha sikupaswa kutaja adharani Kuwa Nasoma
Kwa dhiki, ili iwe ni amasa kwa wanahabari wenzangu ambao hawana
mawazo kabisa ya kujiendeleza kielimu Kuwa ukiamua na ukamtanguliza
Mungu inawezekana.
Mume
wangu 'Rais Mdhurumiwa' Marehemu Dk.Sengondo Mvungi, Profesa
Paramaganda Kabudi,Dk.Harrison Mwakyembe, Mwanangu ambaye ni mtoto wa
Marehemu Dk.Mvungi, ambaye ni Mkuuu wa Kitivo cha Sheria (UB) na Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Dk.Natujwa Mvungi hawa wote walikuwa ni
waandishi wa Habari tena bora na DK. Mwakyembe na Dk.Natujwa walisomea
kozi ya uandishi wa Habari lakini marehemu Dk.Sengondo Mvungi hakuwahi
kusomea chuo chote kozi ya uandishi wa Habari licha alikuwa ni
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mzalendo na Dk.Mvungi alipelekwa
kufanyakazi Gazeti la Mzalendo na Mwandishi Mkongwe Ndimara TIgambwage.
Lakini
mwisho wa siku waliamua kukata shauri na kwenda vyuoni Vya elimu ya juu
kusoma fani ya Sheria na Leo hii wamekuwa ni msaada mkubwa kwa taifa
hili Kwani wamekuwa wAkitumiwa na serikali, Jamii kutoa huduma ya
taaluma Yao ya Sheria.
Hivyo
binafsi nikiwa Natazama historia za wasomi hawa, nimejifunza jambo
Moja Kuwa ukiamua kukata shauri kutaka kujiendeleza kielimu unaweza.
Waandishi wenzangu ambao bado hamjakata shauri , hamjachelewa, anzeni
sasa.
Swahiba
wangu Mchungaji Christopher Mtikila tukutanapo au tupigianapo simu
neno la lake la kwanza kuniambia ni "Saa ya Ukombozi...Mimi na Mjibu ni
Sasa".
Mataifa
ya wenzetu yamepiga Hatua za kimaendeleo kwasababu waandishi wao wa
Habari wameweza kwenda shule vizuri na Waandishi wao wengine wameamua
kubobea Katika Nyanja Fulani , mfano Mwandishi wa Habari za mazingira
amesomea kozi ya mazingira hivyo akiandika Habari inayohusu mazingira
anaifahamu vizuri kwasababu.
Kama
kweli waandishi wa Habari wa Tanzania tumedhamilia kulilitetea taifa
letu maendeleo, basi tuzidi kujiendeleza kielimu na ikiwezekana tusomee
fani nyingi tofauti na uandishi wa Habari ili mwisho wa siku uakiamu
kuandika makala au Habari inayohusu labda mambo ya uchumi, Afya , Sheria
unaiandika vizuri tena bila msaada wa Wanataaluma ya ya uchumi, Sheria
au Afya kwasababu Tayari unakuwa unafahamu nini unachokiandika kwa
mujibu wa taaluma hiyo.
Naamini
tukiamua kujiendeleza kielimu miongoni mwenu 'mtakataa kugeuzwa geuzwa
Kama chapati' na baadhi ya wanasiasa na Makundi mengine yenye Fedha
ambayo ya natumia Fedha zao kuwahonga baadhi ya waandishi wa Habari
kuchapisha Habari ambazo hazikidhi vigezo na zenye Lengo la kuchafua
watu wengine.
Mwisho
Nawashukuru wale wote walionishauri niende kusoma Sheria Kwani Leo hii
naona faida ya ushauri wao kwani nimeweza kupanuka kifikra na kuwa imara
katika fani yangu ya uandishi wa habari.Mungu awabariki sana.
Imeandaliwa na ;
Happiness Katabazi
Ofisa Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB),
Mwanafunzi wa Mwaka wa pili wa Shahada ya Sheria(UB)
0716 774494.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Agosti 29 Mwaka 2014,
0 comments:
Post a Comment