Tuesday, July 8


mgahawa
Jumatatu July 07 kwenye moja ya migahawa iliyopo eneo la Uzunguni Jijini Arusha,Watu wanane waliripotiwa kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu.
Mkurugenzi wa makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi Kamishina Issaya Mngulu amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa nane usiku ambapo watu wasiojulikana walirusha bomu hilo ndani ya mgahawa ujulikanao kamaVama Traditional Indian Cusino uliopo jirani na viwanja vya Gymkhana jijini Arusha.
Pamoja na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Jeshi la Polisi za kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na usalama na yenye tulivu,bado kumeendelea kuwa na matukio ya kiuhalifu yakiwemo ya milipuko katika maeneo mbalimbali.
Mkurugenzi wa makosa ya jinai anasema>>“Kufuatia kutokea kwa matukio haya bado tunaendelea na upelelezi wa kina ili kuhakikisha kwamba wale wote walioko kwenye mtandao huo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo  vya sheria’
‘katika tukio hilo la jana tayari watu wawili wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi lakini pia kati ya wale wanane mmoja wao hali yake siyo nzuri hivyo amepelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi’.
Pia ameongeza kwa kusema katika matukio mengine ya nyuma yaliyowahi kutokea mpaka sasa jumla ya watu 20 wamekamatwa wakiwemo sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea Julai 3 mwaka huu nyumbani kwa Shekhe Ally Sudi mkoani Arusha na wengine 12 katika tukio lililotokea Zanzibar.
Hata hivyo Kamishina Mngulu ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, vilevile wawe makini na mtu ama kitu watakachokitilia shaka.

0 comments:

-