Saturday, July 26

madaktari wanaokabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone

Serikali ya Nigeria imesema kuwa imeweka hali ya tahadhari katika maeneo yote ya kuingia nchini humo kufuatia thibitisho kwamba raia mmoja wa Liberia alifariki katika hospitali moja ya Lagos akiwa anaugua ugonjwa wa Ebola.
Ni kisa cha kwanza kuthibitishwa nchini Nigeria ambalo ndio taifa lenye idadi kubwa ya watu barani afrika.
Mtu huyo anadaiwa kuwa mgonjwa katika ndege siku ya jumaanne kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa hospitalini ambapo alitengwa.
Waziri wa afya nchini Nigeria Onyebuchi Chukwu amesema kuwa abiria wengine wanafuatiliwa kwa karibu.
Ugonjwa wa Ebola umewauwa zaidi ya watu mia sita magharibi mwa Afrika.

0 comments:

-