Mtoto (kulia jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 anayemtuhumu baba yake kumfundisha uchawi.
MTOTO mmoja
mkazi wa Kimara Salanga, jijini Dar es Salaam (jina limehifadhiwa)
mwenye umri wa miaka 12 hivi karibuni aliibuka na kutoa madai mazito,
akimtuhumu baba yake mkubwa kuwa alimfundisha uchawi, Ijumaa lina mkasa
kamili.
Akizungumza
na gazeti hili hivi karibuni, mtoto huyo alisema alianza kufundishwa
tabia hiyo mbaya na baba yake mkubwa wakati huo akiwa na umri wa miaka
mitano jijini Mbeya, kwa kumwelekeza namna ya kuroga na kuua watu.
Katika mojawapo ya matukio
makubwa aliyodai kuwahi kuyafanya ni pamoja na kutengeneza ajali ya boti
iliyotokea Nungwi mapema mwaka huu ambapo yeye na wenzake walitumwa na
baba yake huyo kutega mambo yao huku wengine wakipanda kwenye chombo
hicho ili kuongeza uzito uliosababisha boti hiyo kuzama na kuua watu
kibao.
“Tuligandisha maji na kuweka
sindano ambazo zilitoboa na baada ya watu kufa tulichukua nyama na damu
kwa ajili ya kula na kunywa. Kwa hiyo nimeua na kula nyama za watu.
Baadhi ya tunguli za uchawi zilizokuwa zikitumiwa na mtoto huyo.
“Pia
niliwahi kutumwa kwa msichana ambaye nilimnyunyizia dawa, nikamkalia na
kumkaba shingoni mpaka akafa, nikamchukua na kumpeleka kwa baba mkubwa,
pale kitandani niliacha gogo ambalo lina sura yake, kule tulimla na
kunywa damu yake sisi na wachawi wenzetu.
“Baada ya
kufanya matukio hayo mazito, baadhi ya wananchi waliponigundua kuwa ni
mchawi, walienda kunishtaki kwa mama yangu mzazi, wakimwambia
asiponihamisha wataniua.
“Kwa hali hiyo, huyu mjomba
wangu akanileta Dar kwa ajili ya kufanyiwa maombi, lakini siku ya kwanza
tu baada ya kufika, wakati nakwenda kuchota maji nilikutana na mmoja
(jina limehifadhiwa) aliyeniambia kumbe mimi ni kijana wa kazi,
alinitambua kutokana na nyota tunayobandikwa kwenye paji la uso baada ya
kujiunga na uchawi ambayo ukikutana na mwenzako mnatambuana.“Baada ya
kuniambia hivyo, usiku wake nikiwa nimelala, baba mkubwa alikuja kichawi
na kunichukuwa na kunipeleka kwa yule mzee ambaye ndiye mkuu wa wachawi
wa eneo hili, akanikabidhi kwake na mikoba yangu ya kichawi na hapo
ndipo nikaendelea na kazi kwa upande wa huku Dar nikishirikiana na
wachawi wengine.
“Kazi
yetu mara nyingi ni kuloga, kuua na kunyunyizia dawa kwenye makaburi,
yakifunguka tunachukuwa nyama za watu na mafuvu na kuyapeleka nyumbani
kwa yule mkuu wa wachawi wa eneo hili tunapokutania.
“Hapa nyumbani kwa mjomba
niliweka dawa kwenye ukingo wa nyumba ili wasimalizie kujenga na kumloga
mkewe ambaye tulimtupia vidonda vya tumbo, nilitaka kumuua lakini
maombi yalimsaidia,” anasimulia kijana huyo.
ATINGISHA KIJIJI CHA SALANGA
Kwa mujibu wa shangazi yake
aliyefahamika kwa jina la Lucy, baada ya kufanyiwa maombi kanisani kwa
Mwingira, mtoto huyo alikiri kuachana na uchawi lakini alikuja kugundua
bado anaendelea kutokana na kufanya maombi ya kufunga ambapo aliona
katika maono kuna dawa ameweka kwenye nguo zake alizokuwa akipenda
kuzivaa kila siku. Alipobanwa kwa vitisho ndipo aliwataja wachawi
wenzake na kuongeza kuwa kila alipokuwa akitoka kwenye maombi, anakutana
na wachawi wanamvisha uchawi tena na ule wa tumboni aliolishwa bado
unaendelea kufanya kazi.
WATINGA KWA MJUMBE WA SERIKALI ZA MITAA
Baada ya kueleza mambo hayo
mazito waliamua kutinga kwa mjumbe ambaye baada ya kuwasikiliza
aliitisha kikao cha pamoja na yule mzee ambapo mtoto huyo alieleza
kinagaubaga mbele ya wananchi mambo wanayofanya wakiwa na mzee huyo
lakini alikataa na kuapa kwa kutumia msahafu kuwa anasingiziwa na kwamba
hajawahi kufanya mambo hayo.
NYUMBANI KWA MZEE ANAYEDAIWA MCHAWI
Mapaparazi wetu walitinga
nyumbani kwa mzee huyo ili azungumzie suala hilo lakini jitihada
ziligonga mwamba baada ya kumkosa ambapo mkewe anayedaiwa kushirikiana
naye kwenye mambo hayo, aliyejitambulisha kama mama Isha, alisema; “Ni
kweli huyo mtoto alieleza mambo hayo kwa mjumbe lakini naapa kwa jina la
Mwenyezi Mungu, mimi na mume wangu siyo wachawi, hayo ni maneno ya
uzushi tu, watu wa kijiji hiki wanatuonea wivu kwa sababu tuna maendeleo
kwani hawapendi mtu awe na mafanikio,” alisema.
0 comments:
Post a Comment