Wakati
ikijiwekea rekodi ya ushindi asilimia 100 katika michezo yake yote
kwenye kombe la dunia mpaka sasa wakiwa wamefika katika hatua ya robo
fainali, timu ya taifa ya Uholanzi ambayo ilikuwa ikipewa nafasi ndogo
sana ya japo kuvuka hatua ya makundi, wameahaidiwa zawadi kubwa sana na
ya kipekee ikiwa tu wataweka historia ya kutwaa ubingwa wa dunia kwa
mara ya kwanza.
Kampuni ya masuala ya anga ya nchi hiyo
iitwayo Ruimtevaartbedrijf SXC aerospace engineering company imeihaidi
timu ya taifa ya nchi hiyo safari ya kwenda mwezini ikiwa tu
watafanikiwa kubeba ubingwa wa dunia..
Mmoja wa wahasisi wa SXC Michiel Mol alikiambia chombo cha habari cha Uholanzi, NL Times:
“Kama kampuni yenye asili ya kidachi, tunayo
furaha kubwa sana na mafanikio ya timu yetu huko Brazil. Kwa kiwango
kizuri wanakionyesha basi wanastahili pongezi za aina yake.
“Tutajaribu kuwapeleka wachezaji kwenye kilele cha umbali wa – 103 km!
“Tutawachukua wachezaji wote 23 na kocha Louis van Gaal.”
NL Times wanaripoti kwamba, kampuni ya SXC
kwa sasa inafanya matangazo ya ndege kwenda mwezini kuanzia mwakani, na
kama kila kitu kikienda kama kilivyopangwa na Udachi wakachukua ubingwa
wa dunia – basi kikosi kizima cha Udachi kitapata zawadi yao mwaka 2016.
0 comments:
Post a Comment