Monday, July 21


Akaunti ya Twitter ya jeshi la Kenya pamoja na ile ya msemaji wa jeshi hilo imevamiwa na wanaharakati ambao wanaonekana kupinga ufisadi.
"Nyote ambao mmeiba pesa za wakenya , tunawaandama,'' haya ndio maandishi yaliyokuwa yamewekwa kwenye mtandao huo.
Kikundi cha wavamizi wa mtandao Anonymous,ndio wamekiri kuwajibika na uvamizi huo.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa 
Meja Emmanuel Chirchir, hutumia akaunti yake ya Twitter kutoa taarifa kuhusu kundi la Al Shabaab.
Wavamizi hao walikosoa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta wakisema kuwa inajali tu masilahi ya watu wenye ushawishi na haifanyi kazi ya kutosha kukabiliana na uwindaji haramu pamoja na dawa za kulevya.Mwaka jana kikundi cha wavamizi wa mitandao wanaojiita Anonymous, walivamia mtandao wa wizara ya ulinzi ya Zimbabwe, na pia kuvamia mtandao wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC. 

0 comments:

-