Michuano
ya kombe la dunia inatarajiwa kuanza siku ya alhamisi wiki hii nchini
Brazil kwa ufunguzi wa mechi kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia,
lakini kama ilivyo kawaida kabla ya mechi husika ya ufunguzi kunakuwepo
na sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo mikubwa. Mwaka huu wasanii
Jennifer Lopez, Claudia Leitte na Pitbull walipangwa kutumbuiza.
Lakini kwa mujibu wa taarifa zilizopo
ni kwamba JLO amegoma kwenda kutumbuiza kwenye sherehe hizo za ufunguzi
pamoja na kwamba ndio msanii alioimba wimbo rasmi wa michuano hiyo.
Staa huyo ambaye wiki iliyopita ameachana na
mpenzi wake Casper Smart – leo hii jina lake halikuwemo kwenye listi ya
wasanii watakaosindikiza sherehe za ufunguzi alhamisi hii.
Kwa mujibu wa FIFA, Jennifer Lopez
hatotumbuiza kwenyey sherehe hizo kutokana na ‘sababu za kiufundi’
ambazo hazikufafanuliwa ni zipi.
Hata hivyo wasanii wengine walioshirikiana na
JLO kuimba wimbo wa ‘Ole Ole’ – Pitbull na Claudia Leitte watapafomu
kwnye sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment