MPENZI msomaji, wiki hii ni kwa walio ndani ya ndoa na wale
wanaotarajia kuingia kwenye ndoa. Ukiona ndoa imedumu kwa miaka mingu
siyo bure na ndiyo maana leo nimeona niwaletee mbinu 3 madhubuti ambazo
zinaweza kuifanya ndoa yako idumu milele. Muamini, akuamini!
Uaminifu ni kitu cha msingi sana kwa wanandoa, unaposhidwa kumuamini mwenza wako mara nyingi sana utakuwa ukidhan anakusaliti kwa kuwa na mtu mwingine hata kama unavyodhani vinaweza vikakosa ukweli ndani yake.

Hali
hiyo inaweza kukufanya ukakosa raha kila mwenza wako anapokuwa mbali na
wewe. Si kukosa raha tu anapotoka ama anapokuwa mbali na upeo wa macho
yako bali pia anaporudi unaweza kushindwa kuonesha upendo wako kwake na
kuweza kujenga chuki dhidi yake.
Amini kwamba mwenza wako ni mwaminifu kwako na jijengee mazingira
ambayo na yeye ataamini kwamba wewe ni mwaminifu kwake. Muamini ili naye
akuamini. Epuka sana kufanya mambo ambayo yanaweza kumsababishia mwenza
wako akadhani una uhusiano wa kimpenzi na mtu mwingine nje ya ndoa.
Waweza kufanya hivyo kwa kuwa makini na maneno yako pamoja na matendo
yako ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kudhihirisha kwamba
siyo mwaminifu katika ndoa.
Kitendo cha kuchelewa kurudi kazini kila siku bila kuwa na sababu za
msingi, kulala nje, kuwa na uhusiano wa karibu na watu jinsia tofauti
bila kuwepo na sababu za msingi, kupunguza mapenzi, kutokuwa na heshima
ni baadhi ya matendo ambao yanaweza kuonesha kwamba siyo mwaminifu hivyo
ni vyema ukaepukana navyo.
Usiwe mbishi
Watu wana tabia tofauti. Kuna wengine wana tabia ya ubishi hata kama jambo linalozungumziwa halistahili ubishi. Kama utakuwa na tabia hiyo basi ni vyema ikaishia nje ukiwa unabishana na wenzako kwa kufurahisha genge.

Tambua kwamba mabishano hayana nafasi katika ndoa.
Unapokuwa na tabia ya kubishana na mpenzi wako hata katika kile ambacho hakistahili kubisha, fahamu unakaribisha mazingira ya kuwepo kwa ugomvi.
Unapokuwa na tabia ya kubishana na mpenzi wako hata katika kile ambacho hakistahili kubisha, fahamu unakaribisha mazingira ya kuwepo kwa ugomvi.
Kama kweli unataka kuona ndoa yenu inakwenda vizuri jifunze ukweli
kwamba siyo kila wakati unaweza kuwa sahihi, kuna wakati utakuwa hauko
sahihi na inapotokea hivyo basi kubaliana na hali halisi kisha omba
msamaha.
Wazazi wetu wamekuwa mara nyingi wakitufundisha kwamba kumbishia mtu
aliyekuzidi umri ni dalili za kutokuwa na heshima.Hivyo hivyo kwa
wanandoa, unapombishia mwenza wako inaonesha kwamba haumheshimu tabia
ambayo inaweza kusababisha nyufa katika ndoa yenu.
Maneno ya watu ni sumu
Hivi unajua kwamba kuna baadhi ya watu hawapendi kuwaona wenzao wakiwa katika ndoa yenye furaha na amani?Watu hawa ndiyo wanaosababisha kuvunjika kwa ndoa nyingi. Maneno ya watu ndiyo yamekuwa yakijenga ama yakibomoa ndoa nyingi hivyo basi sikushauri usiyasikilize kabisa, japo yapo yenye maana.

Anapokuja mtu na kukuambia amemuona mume wako ama mke wako na mtu
mwingine, kwanza jiulize mtu huyu ana lengo gani? Hivi lengo lake siyo
kukutaka umuache kweli, endelea kujiuliza kwamba ndoa yenu ikivunjika
ama ikiwa katika machafuko yeye aliyekuletea taarifa hizo atafaidika na
nini? Kwa kifupi hakuna.
Ndiyo maana nasema, unayoambiwa na watu yachuje kwanza kabla ya
kuyafanyia kazi sio kila unaloambiwa unakimbilia kuchukua uamuzi. Maneno
ya watu mara nyingi yanasababisha kuvunja ndoa za wengi kama siyo
kusasabisha machafuko katika ndoa hivyo ni vyema ukaepukana nayo.
Kabla ya kumalizia mada hii niseme kwamba kumekuweo na malalamiko ya
mara kwa kwa wanandoa ambao wote wanafanya kazi juu ya
uaminifu.Tunafahamu kwamba ikitokea bahati mkaoana wote mnafanya kazi
uvumilivu wa hali ya juu unahitajika bila uvumilivu ndoa itavunjika
mara moja.
Ndiyo maana tumekuwa tukishuhudia ndoa za watu matajiri zikiwa katika matatizo makubwa. Itaendelea wiki ijayo
0 comments:
Post a Comment