Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, mpango kwa ajili ya
kuachiliwa kwa baadhi ya wanafunzi wa kike waliotekwa nyara nchini
Nigeria unakaribia kufikiwa wakati serikali ya Nigeria ikiitisha mpango
wa makubaliano.
Baadhi ya wasichana walitarajiwa kuachiwa huru kwa kubadilishana na wafungwa wa Boko Haram.
Kundi la Boko Haram limewateka zaidi ya wasichana 200 waliokuwa
shuleni Aprili 14 mwaka huu na kuamsha hisia kali miongoni mwa watu
wengi wakiwemo viongozi wakubwa
duniani.
Serikali ya Nigeria iko chini ya shinikizo la kufanya juhudi zaidi
kwa ajili ya kukabiliana na kundi la Boko Haram ambalo limewateka
wasichana hao.
Maelfu ya watu wamefariki tangu kundi la Boko Haram lilipoanza kampeni ya nguvu dhidi ya serikali ya Nigeria mwaka 2009.
0 comments:
Post a Comment