Hii
ni stori nyingine tena ya 2014 ambayo inaingia kwenye list ya zile
stori ambazo ukishaisoma au kuipata unaanza kufikiria mara mbilimbili na
kujaribu pia kutengeneza picha yako mwenyewe kama upo eneo la tukio.
Watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili
kuangalia kama ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana
kwenye kesi inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Imetokea Kenya ambapo jamaa alikua amepelekwa Mahakamani Makadara
Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumaka
Mwanamke aliekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.
Mshukiwa huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka
tisa April 2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani
tena kwenye
eneo la wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini
kwenye purukushani zake hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.
Shughuli za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea
ambapo baada ya hapo Mwanamke alietaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi
karibu naye na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali
nikidhani ni mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya
kunisukuma nikaanguka sakafuni
Baada ya hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe
ndugu yake akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka
kwa sababu ya kesi ya ubakaji.
Hili linakua tukio jingine mimi kulisikia mwaka 2014 la kituko
Mahakamani baada ya mawili ya Mwanza ambapo moja ni Mahabusu kujipaka
kinyesi na kujaribu kutoroka akidhani hiyo mbinu itasaidia mtu
asimshike, mwingine ni alievua nguo zote kushinikiza atendewe haki kwa
kisa cha mauji alichobambikiwa.
Kituko kingine ambacho kilivunja rekodi kabisa ni cha Wafanyakazi
wawili wa Mahakama nchini Italia kufanya Hakimu kuahirisha kesi baada ya
wawili hao kuonekana wakifanya mapenzi kwenye chumba cha pili pembeni
ya chumba kilichokua kinaendeshewa kesi.
0 comments:
Post a Comment