Akiwa kwenye harakati zake za kwenda kwenye show uingereza Davido
alifika airport na passport yake ya Marekani.Maafisa wakamwambia alete
passport ya Nigeria kwasababu passport hiyo ya Marekani haikuwa na
karatasi za visa ya kuingia Nigeria kwa hiyo utaratibu haujafuatwa.
Davido alisisitiza kwamba anayo passport ya Nigeria lakini ameiacha
nyumbani. Hakuruhusiwa kusafiri hadi hiyo passport ya Nigeria
ilivyoletwa na akaruhusiwa kusafiri. Baada ya hapo ali-tweet akiwatusi
maafisa wa hapo airport kwa kile kilichotokea.
Ofisi
ya maafisa wa uhamiaji wamesema tabia kama hiyo ya bwana Davido Adeleke
sio sawa kabisa kwasababu afisa huyo alifata utaratibu wa kazi ambao
umesaidia Davido. Huko mbele ya safari angeweza kurudishwa au kuaibika
zaidi kwani kwenye airport nyingine ambapo utaratibu unafatwa kwa hali
ya juu wasingemruhusu kuendelea na safari.
0 comments:
Post a Comment